Makavu live kwa mnaoenda vyuoni

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
748
Reaction score
367
Oyaa! Halafu nyie jamaa mnae soma elim ya juu kwa fedha za mikopo halafu naomba mjue kwamba hzo ni kodi zetu kwahiyo mpango Wa kua na sim za laki 8 hata laki 3 tu Mimi naona mnazingua lakin pia inasemekana mnaongoza kwa kuhudhulia club na sehem nyingine za starehe.

Pia inasemekana kuna michezo michafu saana huko vyuoni ya kufundishana MTU anapokua kilaza kwamfano MTU akiwa na hela anaweza kua ndio mwenye matokeo mazuri darasani lakin akina Dada warembo pia mnakua na matokeo mazuri kwa mbinu maalum.

Halafu kumbe wakati mpo vyuo mnajidanganya saana eti ooh ukitoka na cheti chako tuu Kazi nje nje. Sasa kama bdo upo chuo nakuomba badili kabisaaa mwenendo huku mtaani kumenuka vyeti baadae saana kwanza uwezo wako na kujituma sasa ujinga Wa kugoma mkitaka mikopo kumbe mnamaliza kwa kuwa honga ma professor na ma genius ili wawasaidie huku hajuna hiyo.

Nilikua najiuliza kwanini makampuni yanaona bora yaingia ghalama kuajiri watu toka kwao? Kumbe wamegundua sisi hapa ubabaishaji mwingi vyeti vizur Kazi ovyooooo.

Mna shinda mliman city na kwenye majumba ya starehe achani hizo kitu tunahitaji wasomi wengi saana ili kulikomboa taifa hili . Kwasababu mpaka sasa linaongozwa kiuzoefu na ili liongozwe kiutaratibu na kisomi tunahitaji akina January makamba, mnyika, kafulila, mdee, sugu , zito wengi saana vinginevyo tutaendelea kuburuzwa hiv hiv.

Nashangaa mmejaa hapa Jf mnalalamika kila siku na nyinyi ni wasomi je sisi std seven tuseme nini? BADILISHENI MTAZAMO MTUSAIDIE.
 
Sijui ni kwa nini baadhi ya Wanajamii wana chuki na Wanavyuo!?


Anyway!! Tutafika tu!!
 
Karibu kwenye maandamano jua likiinuka.
 
kwani hizo hela tunachukua bure!?? huwa tunasaidiana kuzirudisha bodi wakianza kukata mishahara yetu.... my money my life, ata nkiamua kuzifanya toilet pepa ni zanguuuuuuuuu
 
Nitakufananisha na MTU ambae anaacha taa ya umeme inawaka mchana kutwa eti kwasababu umeme si ninanunua mwenyewe? Hatuhitaji wasomi wenye kufikilia kuhusu wao fikiria juu ya wazee na wasio jiweza soma uje kuwasaidia mkuu.

#King #mtesa huko u.meenda mbali kwaupande wangu nawachukia wasomi wote wenyetabia tajwa na pia nimezidi kuhudhunika nilipo pata tathimini ya 68% ya wahitim hawana ubora Wa kukabiliana na soko na ajira halafu MTU anasema oooh nikiajiliwa si nitakatwa hela wakati uwezekano Wa kupata Kazi mgum kwa tathimin hyo. Au ukifanya biashara au ukiwa konda Wa daradara serikali itakuona ichukue hela uliyokopa? Kueni na uchungu kidogo basi kaka zetu.. mkiingia mtaani kutafuta Kazi mkikutana na wakenya mnakosa Kazi coz wao wana 46 % ya wahitim wapo vizuri sokoni.
 
Tatizo la ajira linaangamiza vijana wengi,serikali panueni wigo wa ajira muokoe jahazi
 
Eti#handsime boy?
Any way vyovyote utakavyoita poa tuu! But massage sent au!
 
#Wakaya inaonyesha unacho kijua we we juu ya neno elimu ni kupita mabanda meengi na kua na vyeti si ndio? Kama upo hivyo hakika nitakua nakosea lakini kaa ukijua kwamba ELIM NI KILE KINACHOBAKI KICHWANI BAADA YA KUSAHAU YOTE ULIYO JIFUNZA DARASANI.
 
Pole sana...wenzio walivyokuwa wanasoma hadi wakafika chuo wewe ulikuwa unacheza kombolela? Inaonekana uelewa wako ni mdogo sana kwa nini usingetafuta hata jirani yako akakupa dondoo mbili tatu kuhusu chuo? Mtu akiwa na simu ya laki tatu chuo ametumia juhudi binafsi nje ya mkopo....achilia mbali hiyo ya laki nane? Tatizo mkiwa huko mtaani mnajazana pumba sana kuhusu chuo? Hivi profesa mzima atake hela yako ili akufaulishe kwa njaa gani aliyonayo?

Unapata mkopo kiasi gani labda....Kwanza wewe mwenyewe kwa hela gani uliyonayo? Wengine hadi wamalize degree zao wanakuwa wamesoma kozi karibia hamsini....zote hizo amefaulu kwa kuhonga hivyo vijihela vya bodi? Punguza chuki ndugu...kama unaumia watu kula hela ambayo hata hivyo watairudisha somesha watoto wako na wewe ili waje wale......kwa mawazo hayo uliyonayo ukipeleka mtoto chuo utaacha hadi kufanya kazi usubirie mkopo wa mwanao ukulishe.
 

Ndugu yangu kusoma mpaka kufika chuo ni fursa. Usije ukamuhukumu hata siku moja eti kwann huyu hajafika chuo.

Wewe uliyebahatika basi shukuru. Kunawengine walikuwa na nia kabisa lakini walishindwa eidha kwa sababu za kiuchumi au kiutamaduni na mila.

Katu usijisifu katika hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…