The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kutokana na kitongoji cha Dombwela kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe kukubaliana kujenga ofisi mpya za kitongoji hicho, wananchi wamekubaliana kubadilisha sheria kwa watakaokuwa hawafiki kwenye mikutano ili irahisishe shughuli za ujenzi huo
Katika mkutano wa kitongoji hicho uliofanyika Machi 1, 2025 Mwenyekiti wa kitongoji hicho Joseph Mbilinyi amewaeleza wananchi hao kuwa wamepatiwa kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi za kitongoji na tayari zaidi ya shilingi milioni 4.1 zimechangwa na wadau kufaninisha ujenzi huo hivyo kila mwananchi atachangia shilingi 5000 kwa ajili ya ujenzi huo
Mwenyekiti huyo amewaomba wananchi kuridhia ombi lake la kutoza shilingi 5000 kwa ambaye hajafika kwenye mkutano na badala yake kwa kuwa wana ujenzi wa ofisi, kwa anayeshindwa kufika alipe mfuko mmoja wa saruji
Baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu pendekezo hilo la Mwenyekiti wakisema faini hiyo inayopendekezwa ianze kutozwa kwenye mikutano inayokuja, na kwa walioshindwa kufika kwenye mkutano wa jana watozwe faini ya shilingi 10,000 badala ya 5,000ya awali,huku wengine wakianza kutoa michango papo hapo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo
Hivyo wananchi hao wamekubaliana kutoza mfuko mmoja wa saruji kwa wananchi watakaoshindwa kufika kwenye mkutano bila ruhusa, sheria itakayoanza kutekelezwa mara moja.