Making it a BETTER place..........

kande kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2011
Posts
234
Reaction score
88
Wadau,

Nikiri kuwa mimi ni mpenzi mkubwa wa nachi nachi, mapicha ya sinema ya kihindi. Sababu kubwa ya kupenda, mbali na stori, ni yale mazingira ambayo jamaa hutujalia kuyaona( miti/misitu,maua/mashamba ya maua,mandhari maridhawa na mwanana).Na mara nyingi scene za kwenye hayo mazingira, huwa ni kuhusu mapenzi at its peak!

Si bahati mbaya kuwa mazingira hayo huambatanishwa na mambo ya mapenzi, lakini ukweli ni kuwa mazingira ni chombezo,tiba na mjenzi wa mapenzi. Hapo mtazungumza hali yenu ya mapenzi,mtatatua migogoro nk.

Hivyo basi nawasihi tuyaweke mazingira yetu sawa/muafaka pamoja na sababu nyinginezo,lakini kwa mapenzi pia.Tupandeni miti masika hii kwa wingi. Hebu tuone fahari katika kufanya hili.

Tupande miti tuirudishe dunia angalau kidogo katika hali yake ya asili, iwe sehemu bora kuishi, sehemu bora kwa ajili ya kusadadisha mapenzi.

Over.
 
haya, asante kwa kutukumbusha kupanda miti.

Siamini katika mapenzi ya kihindi maana ni ya kiongo mno. Stering anachomwa jambia kwenye koromeo afu anaamka anaimba kwenye maua?
 
Thaaank yu sana kwa advice...japo kuwa suala la kupanda miti ni mtihani kibongo-bongo..ule mwamko hatuna.
 
haya, asante kwa kutukumbusha kupanda miti.

Siamini katika mapenzi ya kihindi maana ni ya kiongo mno. Stering anachomwa jambia kwenye koromeo afu anaamka anaimba kwenye maua?

Hahahaahahahahahahaaaaaaaaaaaa! My dia umesahau kuwa stering hauawi........lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…