MakJuice ni Upotoshaji unaoota mizizi Tanzania

Hehe heee

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2017
Posts
213
Reaction score
186
Kuna hii mentality moja TZ kwamba kila anayeanzisha juice Point yake basi kaiga kwa Makjuice nachukizwa sana na hili.

Niwaekeweshe tu: Juice bar zipo kitambo TZ na ni nyingi sana ila Makjuice ni jamaa kapata umaarufu tu kwenye biashara hiyo kwa sababu ya kuji brand na network kubwa aliyon ayo na anayoifanya. Kwa hilo apongezwe, ila juice bar zipo TZ especially DSM tangu yeye yupo anasoma.

Chakuongeza pia Dunia ime exist miaka mingi sana kiasi cha kwamba hakuna tena idea mpya na kwa TZ sasa hivi idea nyingi tunachukua nje.

Mfano, Starbuck ni biashara inayofanya vizuri kwenye soko, sasa hivi inaingiza billions of money. Binafsi nina wazo la kukopi kuifanya TZ ila sina power kwa sasa. Sasa akitokea mwingine mwenye uwezo wa kuifanya akajulikana then Mimi nikija kufanya itakuwa nimeiga kwake.

Hili suala naliona hadi kwa Manara eti kamuiga Diamond sijui mwana FA, jamani viumbe hai idea hizi zipo toka wote humu hatujazaliwa.

Hiyo mifano tu, tuache hii mentality.

Tuache kuishi zama za feudalism TZ dunia inaenda fasta sana.

NB: Upo karne hii na huna ndoto ya kufanya biashara ya kuanzia 100M kwenda juu, nakusalim.
 
Huyo jamaa nishewahi kuangalia interview yake YouTube.

Kiukweli amenishangaza sana yani utazania Juice hapa Tanzania amaenza kutengenez yeye wakati zimeanza tangu zaman.

Ushauri...anachotakiwa kufanya kuwa postive way katika kuona ni namna gani anaweza kulikamata soko.


Ushindani katika biashara ni jambo lakawaida sana anachotakiwa kutafuta jinsi gani anaweza kushindana lakn asianze kujiona Vistm kwamba kuna ma-Done wameingilia kazi yake..


Sent using Samsung Galaxy Note7
 
Hapo kwa haji manara nafikiri yeye perfume yake ni kawalenga zaidi watu wenye ulemavu wa ngozi au ni kwa ajili ya wote?
Halafu kuhusu perfume ya diamond ipo sokoni kweli maana hata sisikia akiifanyia promotion
 
Mkuu naomba maujuzi namna ya kutengeneza hizi juice, maandalizi yote yani.
Mabungo-
Unatoaa mbegu zile,una saga na blender,
Unachuja mbegu na kichujio,ile juice nzito ya mabungo iliyotoka kwenye tunda za ndani una mix na maji yaliyochemshwa una changanya na Sukari....juice ya bungo tayari

Ubuyu hivyo hivyo au unaweza chukua ubuyu ukaziloweka baada ya Muda Unachuja mbegu za ubuyu na kubaki maji mazito ya ubuyu una mix na maji na Sukari,juice tayari

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…