Makocha huwa wanafundishwa upofu huko vyuoni wanakosomea ukocha?

Makocha huwa wanafundishwa upofu huko vyuoni wanakosomea ukocha?

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Awali nilikuwa najiuliza kuwa kama hawa ndio wazungu na ndio inaaminika wao ni binadamu wenye akili kutuzidi! Inakuaje wanashindwa kuona vitu ambavyo viko wazi kabisa kwenye football!?

Vitu ambavyo mtu wa majohe huko ndani ndani na hana hata Leseni F ya FIFA anaona lakini wao hawaoni kuanzia kwenye sajiri mpaka maamuzi kwenye timu.

Nimeshuhudia makocha wengi sana wa Ulaya tena timu kubwa wakifanya maamuzi ambayo kocha Mkombe wa gongo la mboto jeshini hawezi kuyafanya kabisa na hua yana wacost wanafungwa.

Hii hali imenifanya nitamani kujua huko wanako somea ukocha hua wanafundishwa vitu gani vinavyo vina watia upofu kiasi hiki.

Msimu wa 2018-2019 Dunia nzima ilikua inaona kua muokozi wa Tottenaham Hotspurs ni Lucas Moura

kasoro kocha mkuu wakati huo wa Spurs Mauricio Pochetino imagine Dunia nzima iliona hilo kua Lucas alikua form na ndio mhimili muhimu kwenye timu kwa wakati ule, kasoro kocha mwenye grade A ya leseni ya ukocha ya FIFA.

Yeye ndie aliewapeleka nusu fainali pia yeye ndio aliwapeleka fainali alikua wamoto sana ila siku muhimu na ya kipekee ya fainali Maurocio Pechetino akampiga bench aka anza na Harry Kane aliyekuwa majeruhi, ukiuliza kwanini hakuna anayejua.

Hata mashabiki wa Liverpoool walifurahi ile siku kuona Moura haja anza.

Kwenye robo fainali muhimu tena inayo hitaji magoli mengi Kocha mkuu wa Simba SC Tanzania Didier Gomes ana msimamisha Mugalu mbele.

Dakika zote 45 za kwanza Dunia nzima hadi wamama wasio na ufahamu mkubwa wa soka waliona kua mshambukiaji huyo alikua ni mzigo kwa timu cha ajabu Gomez alikua haoni! Hakuona kabisa yani,,,Mugalu akamaliza mpaka dakika 90 wakatupwa nje ya mashindano, ajabu sana hii.

Usiku wa jana Manchester United ilikuwa Poland kwenye fainali ya EUROPA League napo yale yale ya upofu wa makocha nika yashuhudia.

Kwenye footaball kuna Kitu kinaitwa Duo, yani watu wawili wa eneo fulani walio elewana vyema.

Bila shaka na kupepesa macho duo bora ya manchester united msimu huu ni ya Fred na Mc Tominay imefanya vyema sanaa msimu huu Pia kupitia hii Duo imefanya hata Pogba kwenda juu kama kiungo wa pembeni na amekua bora sana kwenye mechi mbili tatu alizo cheza huko huku akikabiwa na duo takatifu.

Wakati Duni ikiona haya Ole yeye alikua kipofu na hakuonaa kabisa hilo, siku ya fanali muhimu anaweka Fred bench na anamrudisha Pogba chini, sasa una baki ushangaaa hawa watu hua hawataki kushinda!?

Baada ya dakika 20 tu! za fainali hii ya Europa kila mtu aliona kua Rashford alikua ni mzigo na hakua na msaada zaidi ya kuchosha wenzake

Hata hili pia Ole alikua kipofu na hakuona. Rasford alimaliza 120 zote! Huku wakitolewa wakina Greenwood na Eric Bailly walio onekana kuwa na msaada zaidi yake.

Kuna maajabu ya upofu wa makocha yanaendelea mpaka yana nifanya nitamani kwenda kusoma ukocha ili nikaone hua wanafundishwa litu gani kinacho watia upofu wa kuto ona vitu vinavyoo onekana bila lenzi!

#Ggmu

IMG-20210527-WA0046.jpg
 
Maelezo mazuri mkuu.

Rekebisha tu hapo ulipoandika 'awari' na 'mhimiri'.

Halafu ile mechi ya mnyama juzi haikuwa nusu fainali mkuu.

Big up.
 
Nimesikitishwa sana na mwandishi huyu ambae kwa namna moja ama nyingine zile sheria mpya ya sub 5 za fifa kwa kipindi hiki cha Corona kuona kabisa aliyezitunga alikuwa professor Didier Gomes Da Rosa.
 
Nina kauzoefu kidoogo ka kukaa benchi ama kuiongoza timu.. Mtaani kwangu walifikia kuniita Diego simeone.. Chama langu nishalifikisha fainali 3 (2 tukibeba)

Aisee lile joto la pale benchi liache kama lilivyo mzee, hasaa timu ikiwa inaongozwa. Ni habari ndefu mkuu,

Kikubwa pia huwa naona makocha ni binadamu, kukosea ni kawaida.. Wakat mwingine huyo huyo akianza anakukera, ila akiingia sub anakuonesha kitu, au mazoezini haoneshi ubora ila mpaka akiingia kitu ambacho coach anaweza kuona km kabaahatisha.. Sikumbuki msimu gani ila kuna msimu pale man u game za mwisho mwisho tevez alikuwa anaingia sub anafanya vizuri na alikuwa haanzi 1st eleven, fergie kuulizwa akasema mazoezini haoneshi kama anapaswa kuanza.

2006 fa sijui ni carling ile fainali arsenal vs Chelsea drogba anakuja kutuua mwishoni, Walcott katangulia kufunga, ile game th14 alikuwa kapona, mzee akagoma kumchezesha kisa watoto ndio waliopambana mwanzo mwisho. Dunia nzima ikamlaumu. Inawezekana pochetino angemuanzisha moura na bado wangekufa bado angelaumiwa kwanini kamuacha kane benchi.

Situations zinakuwa tofauti. Ndio maana KAZI YA UCHAMBUZI NI NYEPESI KULIKO UKOCHA.

kwa gomes nilichokiona siku ile nadhani wakat mpira unaanza nilihisi mipango yake, anasubiri wajomba wapaki basi ndio atie bwalya n morisson, mugalu ilikuwa ni kesi nyingine. Angembadilisha baadae sababu kuna game sijui na vita wale alimtoa akamtia kagere.

Ila zile sub za kuumia kwa lwanga na onyango zilimuharibia kila kitu.
 
Nimesikitishwa sana na mwandishi huyu ambae kwa namna moja ama nyingine zile sheria mpya ya sub 5 za fifa kwa kipindi hiki cha Corona kuona kabisa aliyezitunga alikuwa professor Didier Gomes Da Rosa.
Kwamba!?
 
Nina kauzoefu kidoogo ka kukaa benchi ama kuiongoza timu.. Mtaani kwangu walifikia kuniita Diego simeone.. Chama langu nishalifikisha fainali 3(2 tukibeba)
Aisee lile joto la pale benchi liache kama lilivyo mzee, hasaa timu ikiwa inaongozwa.. Ni habari ndefu mkuu,

Kikubwa pia huwa naona makocha ni binadamu, kukosea ni kawaida.. Wakat mwingine huyo huyo akianza anakukera, ila akiingia sub anakuonesha kitu, au mazoezini haoneshi ubora ila mpaka akiingia kitu ambacho coach anaweza kuona km kabaahatisha.. Sikumbuki msimu gani ila kuna msimu pale man u game za mwisho mwisho tevez alikuwa anaingia sub anafanya vizuri na alikuwa haanzi 1st eleven, fergie kuulizwa akasema mazoezini haoneshi kama anapaswa kuanza..
2006 fa sijui ni carling ile fainali arsenal vs Chelsea drogba anakuja kutuua mwishoni, Walcott katangulia kufunga, ile game th14 alikuwa kapona, mzee akagoma kumchezesha kisa watoto ndio waliopambana mwanzo mwisho.. Dunia nzima ikamlaumu... Inawezekana pochetino angemuanzisha moura na bado wangekufa bado angelaumiwa kwanini kamuacha kane benchi...

Situations zinakuwa tofauti.. Ndio maana KAZI YA UCHAMBUZI NI NYEPESI KULIKO UKOCHA.

kwa gomes nilichokiona siku ile nadhani wakat mpira unaanza nilihisi mipango yake, anasubiri wajomba wapaki basi ndio atie bwalya n morisson, mugalu ilikuwa ni kesi nyingine.. Angembadilisha baadae sababu kuna game sijui na vita wale alimtoa akamtia kagere.

Ila zile sub za kuumia kwa lwanga na onyango zilimuharibia kila kitu.
Daah bro kwa game ya jana ya united Ole sidhani kama ana excuse
 
Lakini sub mwisho tano hivyo nafasi ilibaki mbili bado ya sub kwa upande wa Simba
 
Lakini sub mwisho tano hivyo nafasi ilibaki mbili bado ya sub
Inasemekana sheria ya Sub ni 5, ila zinatolewa kwa mikupuo (awamu) 3 mfano unatoa wawili, wawili kisha mmoja, sasa siku zile inasemekana tulitoa lwanga, kisha onyango halafu morrisson kwa mzamiru tukawa tumemaliza mikupuo yetu mi3.
 
Umenikumbusha yule mzee Arsene 'I didn't see it' Wenger. Kama wachezaji wake walicheza faulo na refa hakuona, waandishi wa habari wakimuuliza baada ya mechi kila wakati jibu lake lilikuwa, samahani jamani, na mie sikuona. Ndo jina lake likaboreshwa kidogo kuakisi upofu wake!
 
Back
Top Bottom