Makocha:Mosess Basena Vs Hector Cuper

Makocha:Mosess Basena Vs Hector Cuper

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Makocha wa kiafrika wakiwezeshwa na kuaminiwa wanaweza kabisa leo umepigwa mtanange pale uwanja wa Mandela Jijini Kampala kati ya mabingwa mara kadhaa wa Afrika Mafarao wa Misri na Misri kuchapwa jumla ya goli moja kwa bila lililotiwa kambani na Mchezaji Emanuel Okwi

Uganda ipo chini ya kocha Mzawa Mosses Basena nafikiri wengi tunamjua keshawahi fundisha Simba huyu huku Misri ikiwa chini ya Kocha mwenye mafanikio makubwa sana ngazi ya Dunia Hector cuper Raia wa Argentina na ukiangalia Kikosi chao kilikua kimeshiba langoni akisimama mzee mzima miaka 44 sasa El Hadary,Huyu Salah ambaye aliwafanya kitu mbaya Arsenal,Elneny...nk ila wamefungwa.

Somo Tuwaamini Makocha wetu wazawa kwani wanauwezo Mkubwa
1504197985767.png
tu.

Chini ni Kikosi cha Uganda/Uganda Cranes mchezo ulikua ni kutafuta tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia ukanda wa Afrika

hongereni Uganda.
 
Hongera Uganda.
Inaonekana defence yao ilifanya kazi nzuri hasa Wadada na Juuko.
Pia Okwi kwenye forwards ameonekana kufanya vyema pia.
Hongera kwa Basena na Timu nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
cuper ni kocha mzuri sana. Kama sikosei alishawahi kufundisha hata Inter milan miaka hiyo nasoma shule huku nikiangalia sana serie a lega calcio. Nimiongoni mwa mababu wanaojua sana kufundisha timu na kuinua vipaji. Uganda wameshinda sababu wenzetu kila siku wanakua kisoka alafu wanajua sana kutumia uwanja wa nyumbani. Usishangae kuona wanamaliza wanaongoza kundi.
 
Back
Top Bottom