Makocha Saed Ramovic na Fadlu Davis, walalamikia wingi wa mechi.

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Misimu kadhaa iliyopita kuna wakati aliyekuwa kocha wa Simba Robert Oliveira "Robertinho" na kocha wa Yanga Nasridine Nabi walilalamikia wingi wa mechi na umbali ambao wachezaji husafiri baada ya kucheza mechi na kabla ya mechi inayofuata.

Wote wawili walisema umbali na ukaribu wa kati ya mechi na mechi uharibu ubora wa timu.

Sasa tena makocha wa Simba na Yanga wa Sasa, Fadlu Davis na Saed Ramovic wanarudia maoni yale yale ya makocha waliowatangulia.

Jee Kuna ukweli wowote juu ya madai Yao, kama kuna ukweli nini kifanyike?

Nabi alishauri angalau Kila timu iwe inacheza mechi moja tu kwa wiki
 
Misimu kadhaa iliyopita kuna wakati aliyekuwa kocha wa Simba Robert Oliveira "Robertinho" na kocha wa Yanga Nasridine Nabi walilalamikia wingi wa mechi na umbali ambao wachezaji husafiri baada ya kucheza mechi na kabla ya mechi inayofuata.

Wote wawili walisema umbali na ukaribu wa kati ya mechi na mechi uharibu ubora wa timu.

Sasa tena makocha wa Simba na Yanga wa Sasa, Fadlu Davis na Saed Ramovic wanarudia maoni yale yake ya makochao na waliowatangulia.

Jee Kuna ukweli wowote juu ya madai Yao, kama kuna ukweli nini kifanyike?

Nabi alishauri angalau Kila timu iwe inacheza mechi moja tu kwa wiki
Hakuna ligi yoyote ya maana duniani ambapo timu hucheza mechi moja tu kwa wiki! Hawa makocha wasitafute vijisababu ambavyo haviona kichwa wala miguu!! wakiona vipi wasepe!! Wasikwepe kuwajibika na matokeo kwa kisingizio cha wingi wa mechi!! Wawe wakweli! ligi yetu ni ngumu na wanapewa changamoto ya kufa mtu toka kwa timu zisizo na majina kama vile Tabora United nk!!
 
Wanaona hakuna ulazima wa kucheza mechi mbili Kila wiki.
Sio mechi mbili ni mechi kila baada ya siku 2.Hakuna ligi ya namna hiyo duniani.FIFA wanataka iwe 72 hours siku 3 kati ya mechi na mechi na uwepo muda wa kusafiri.
Geografia ya Nchi yetu hairuhusu kucheza mechi kila baada ya siku 2 ukizingatia usafiri,recovery na muda wa kocha kuthamini kikosi chake.
Ni afadhali kwa timu za Simba, Yanga na Azam na Singida Black Stars zinazotumia usafiri wa ndege.Zilizobaki hali ni ngumu sana.Ratiba sio rafiki kwa quality ya mpira na muda wa kupumzika.Wachezaji sio robots.
 
Umeelezea vizuri na hayo ndiyo maoni ya hao makocha.

Wanasema timu zisizo na uwezo kifedha zinafungwa wakati mwingine kutokana na umbali wanaosafiri kwa mabasi, wingi wa mechi na kukosekana muda wa "recovery".
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Tatizo sio wingi wa mechi ni ratiba za mechi, Simba wametoka kucheza Kagera jumamosi jumanne wanacheza Dar. Kwa sababu wanajiweza wamepanda ndege. Jkt nao wanalalamika hawajapata mapumziko .
Kwa kifupi bodi ya ligi hawajui kupanga ratiba wanaiga ulaya wakati miundo mbinu yetu mibovu.
 
Mimi nashauri ratiba iende hivyo hivyo, ili ligi nayo iwe inamalizika kwa wakati.
 
Tatizo sio wingi wa mechi ni ratiba za mechi, Simba wametoka kucheza Kagera jumamosi jumanne wanacheza Dar. Kwa sababu wanajiweza wamepanda ndege. Jkt nao wanalalamika hawajapata mapumziko .
Kwa kifupi bodi ya ligi hawajui kupanga ratiba wanaiga ulaya wakati miundo mbinu yetu mibovu.
Wamefanya makusudi ili kombe lao la Mapinduzi lichezeke bila kuacha viporo vingi
 
Back
Top Bottom