Freeman Aikaeli Mbowe ni Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (
CHADEMA), amewahi kuwa mbunge wa Hai na mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Desemba 1, 2024
Abdul Nondo alitekwa na watu ambao hawajafahamika katika kituo cha mabasi Magufuli jijini Dar es salaam majira ya saa 11 alfajiri alipokuwa akitokea Kigoma. Taarifa zake zilitolewa na
chama chake lakini pia kupitia kwa aliyewahi kuwa kiongozi wa chama hicho
Zitto Kabwe na baadaye kutoka kwa taarifa rasmi ya jeshi la
polisi.
Usiku wa Desemba 1, 2024
Nondo alipatikana akiwa ametupwa katika ufukwe wa bahari ya hindi maarufu kama Coco beach (kisa kuzima Cha kutekwa na kupatikana kisome
hapa)
Tangu kupatikana kwa
Nondo Polisi wamesema wanaendelea na Uchunguzi Ili kubaini watu waliohusika na Tukio hilo (Soma
hapa).
Leo Desemba 4, 2024 imeibuka Taarifa kwenye Mtandao wa X (Zamani Twitter) yenye nembo ya
Millard Ayo ikidai Jeshi la Polisi limewakamata Makomado wa Freeman Mbowe kwa kuhusika katika kumteka Abdul Nondo, taarifa hizo zimechapishwa
hapa na
hapa.
Ni upi uhalisia wa Taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo haina ukweli na post hiyo haijawahi kuchapishwa na akaunti rasmi ya
Millard Ayo kama inavyoonekana.
Uchambuzi wa Posti husika
Picha iliyotumika kutengeneza chapisho hilo imetolewa katika Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyokuwa inaripoti kuwakamata Watu Waliojaribu kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo na haielezi chochote kuhusu watu hao kuhusika na Freeman Mbowe kama ambavyo Posti
hiyo inadai.
Zaidi ya hayo, Taarifa maalumu ya Polisi inayoeleza kupatikana kwa Abdul Nondo kwenye fukwe za Coco Beach zinaeleza kuwa Uchunguzi wa Tukio hilo bado unaendelea (Soma
hapa), mpaka leo Desemba 5, 2024 hakuna Taarifa nyingine iliyoeleza muendelezo wa tukio hilo
Uchambuzi wa JamiiCheck umebaini aina ya Mwandiko (font type) iliyotumika katika post hiyo haufanani na font anayoitimia
Milard Ayo katika kuchapisha Taarifa zake nyingine.