Makonda, Lissu na Lema

Makonda, Lissu na Lema

Ngokongosha

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2011
Posts
3,400
Reaction score
7,608
Wabunge wa tanzania wamechachamaa baada ya kuambiwa kuwa huwa wanasinzia bungeni.
Maneno ya Makonda yameonekana ni ya dharau na yenye kuzalilisha bunge,

Sioni utofauti kati ya swala la Makonda na lile la wabunge lissu na lema, wabunge hao walipokamatwa kumekuwa na maneno kwamba demokrasia inaminywa, sasa mambo yamewageukia hamana hata anayesema kwamba hii ni demokrasia na Makonda awe huru.

Mimi kwa maoni yangu kama Makonda anakosa basi Lissu na Lema wanamakosa wala tusiwatetee.
 
Kosa la makonda ni sawa na la kina Lissu labda tu ujitoe ufahamu,

Ninaomba kuuliza mnieleweshe.Vita ya Mh.Makonda na Wah.Wabunge katika umoja wao imeanzia wapi.Narudia naomba kueleweshwa.Je ni pale Makonda alipowataja watuhumiwa wa madawa ya kulevya na Mh.Msukuma kuanza kuhoji uhalali wa mali za Makonda?.Kama ndivyo naendelea kuuliza.
Je mali hizi za ghafla za Mh.Makonda ,Mh.Mbunge Msukuma kazijua baada ya Makonda kuwataja wauza unga?
Sielewi nifafanulieni.Je ugomvi wa Makonda na Msukuma ni nafasi zao,unga au mmoja wa waliotuhumiwa ana maslahi binafsi ya hawa wawili?

Sielewi.Tuchukulie wana ugomvi wao binafsi kati yao hawa wawili kipi kina faida kwetu tusio wabunge na tusio wakuu wa Mikoa.Kazi aliyoinzisha Mh.Makonda ina madhara kwa tulio wengi kama Taifa au kazi nzuri Zaidi ni ile iliyoanzishwa na Msukuma?

Nauliza tu ili nielewe.Matatizo binafsi ya hawa waheshimiwa wawili yana athari gani kwa Taifa?

Mniwie radhi nisiyeelewa mimi,nini kimewaunganisha wabunge wote /wengi wao kuunga mkono hoja hii dhidi ya Makonda? Ni kauli za maudhi za Makonda? je ni kupungua kiwango cha maavuno walichotegema kwa kuwa wabunge hakifanani na wanachokipata? ni maslahi mapana ya walio watuma kupitia kura zao?

Tungekuwa na jeuri ya fedha zisizo na matumizi leo tungemwomba Mh.JPM avunje bunge na kuitisha uchaguzi hoja za Wabunge juu ya jambo hili na hoja za Makonda ziwekwe wazi hadharani kwa wapiga kura nani angeibuka mshindi?

Nivumilieni.Nauliza sasa juu ya haki na mgawanyo wa madaraka wa mihimili mitatu.Serikali,Bunge na Mahakama.Makonda kawataja aliotajiwa na waliompa habari kuwa wanashiriki katika biashara ya madawa ya kulevya.Sina uhakika kama kasema wanatumia,wanauza au wanawasaidia wanaofanya biashara hiyo haramu yenye madhara tunayoyaona.Kawaita watoe maelezo kulingana na tuhuma alizotajiwa.Maelezo haya wayapeleke Polisi ili wawasikilize waone kama kuna wanaostahili kwenda mahakamani wapelekwe.Mahakama iaumue.

Mimi ni mmoja wa waliolalamika muda mrefu kuwa hatua hazichukuliwi inavyostahili.Nimeshiriki kusema serikali ianawalea.Je niendelee kumwona Makonda hafai?
Hana kinga yoyote ya kumpeleka mahakamani kama kakosea,kwa nini tuendelee kumtukana na kumwombea kila baya.Likimkuta baya nani asimame badala yake kukemea uovu? Polisi? je hawakuwepo kabla ya yanayofanyika sasa?

Mh.Msukuma yeye kamtuhumu Makonda Bungeni.Makonda hana nafasi ya kujibu hoja bungeni isipokuwa apewe nafasi ya waliomtuhumu.Wao wamemshtaki kawadharau.Wanamwita wamsikilize wao,watoe ushahidi wao na wamhukumu wao.Hii ndiyo aina ya haki tunayoitaka?Kwa nini wasiungane wapeleke malalamiko yao mahakamani maana kwa mwajiri wa Makonda hawaamini kuwa haki itatendeka.

Nielewesheni mbu mbu mbu mie. Naomba kutofautiana na mtazamo wa mlio wengi.Kama ambavyo mlalamikaji hapaswi kuwa hakimu,shahidi ndivyo ninavyo dhani inapaswa kuwa kwa wabunge.Niondoeni eneo ninaloona tofauti na mnayoyaona.

Tafadhali nielewesheni.
 
Kweli huko sahihi hata Mimi naumia sana! MTU anapowatetea watanzania walio wengi wanapinga sijui tumerogwa au akili za watanzania ni maji!Makonda yuko sahihi
 
Back
Top Bottom