Makonda, Next Project Iwe kuwekeza Kwa Vijana kwenye michezo

Tangawizi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Posts
6,696
Reaction score
6,734
Makonda ameanzisha project nyingi sana. Na nyingi hatuna feedback zinaendeleaje sasa hivi. Ila hatujasikia lolote kuhusu kuwekeza kwenye michezo ya vijana kuanza kada za chini kabisa. Ili safari za kwenda kuwatia moyo wachezaji kama alivyoenda Egypt ziwe na tija, ni lazima sasa tusiache eneo hilo pana lenye uwezo wa kuajiri watu wengi, kama la michezo, liachwe bila kupewa msaada wa maana, au kuonyesha kwamba nao wana mchango wa kuchangia kwenye ustawi wa Taifa letu.

Ukianza Dar, wengine wakaiga mfanio, naamini tutaibua na kuendeleza vipaji ambayo vipo, kwa wakati. Ilivyo sasa, hardly watoti wana sehemu za kucheza.Open space karibu zote zimenyakuliwa na watu wenye nguvui. Hakuna msukumo kwenye elimu yetu upande wa michezo.
Sioni namna tutaweza kujivunia matokeo tofauti na yale tunayoyaona kama hali ya sasa itaachwa iendelee. Wachezaji wanatengenezwa. Tuwekeze kwenye viwanda vya kuwatengeneza wachezaji hao, kwenye michezo karibu yote.
Zamani zile kuna mwamba mmoja aliitwa Laurent Gama, alipenda sana michezo. Na popote alipokwenda alijaribu kuhakikisha kuna kitu chenye kuacha alama za kupenda kwake michezo. Ina maana hatuna kina Gama wengine, mpaka siku za kupanda ndege kwenda kushangilia?
 
kamwambie yupo Twitter anabishana na Fatuma karume
 
Tanzania kushindana kisoka na hawa miamba wa Africa bado sana tunahitaji kufanya kazi kubwa sana.
 
Hilo liwe jukumu la TFF zaidi kuliko Makonda!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…