Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amepongeza juhudi za Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.
Akizungumza Alhamisi, Machi 6, 2025, katika Uwanja wa TBA jijini Arusha, Makonda amebainisha kuwa kampeni hii inalenga kusaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kupata huduma za kisheria huku ikiwa haijajikita katika misingi ya ubaguzi.
Makonda ameeleza kuwa Rais Samia ameonesha upendo mkubwa kwa kugharamia kampeni hii, akilenga kuondoa tofauti kati ya wenye nacho na wasio nacho ili kila mtu apate haki yake. Amewasihi wananchi wasiwe waoga kudai haki zao na wasitumie ujasiri wao kudhulumu wengine, bali dhamira zao ziwaongoze kuwa watu wa haki ili kuwawezesha wataalamu kutenda haki.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025