Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,864
- 5,695
Ama hakika nimeona wewe kijana Makonda ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana kiakili. Unaweza kupanga mambo kwa muono wa mbali na yakafanikiwa yaani wewe kwa lugha adhimu ni mwana falsafa.
Mpango ulio kuja nao hivi karibuni wa kutangaza Wagonjwa wa Corona umetusaidia sana wananchi. Baada ya wewe tu kutangaza wagonjwa ugonjwa uliisha pale pale na hakuna kifo wala mgonjwa kuongezeka aisee wewe kweli ni kichwa na mjuvi wa mambo.
Sijui ni kwani yule Waziri wetu wa Afya anakuzuia kutangaza Majina ya wagonjwa wakati anajua kabisa ktk nchi hii, wenye Akili ni wawili tuu unaanza wewe kisha anafuata Kiongozi wa Malaika huko mbinguni.
Wewe hutakiwi kupewa maelekezo maana ni naibu wa Malaika huenda kawaziri kadogo kama hako ka Afya hakakujui kazi zako zingine .Bila shaka Elimu yako wewe ulisomea huko Ulaya ndo maana unafanya mambo kwa weredi sana.
Kwa uwezo wako huo mkubwa kiakili ingefaa uwe unafundisha Chuo kikuu hapo mlimani kuongeza wataalamu zaidi. Lakini kwa kuwa una mambo mengi ya kufanya Yanayo julikana na yasiyo julikana huwezi kupata muda.
Tunakuomba ukikutana na kiongozi wa malaika mkuu, mwambie wanachi malofa wanaomba tuongezee idadi ya Midege walau iwe 600 hivi. Tunataka anga letu lijae midege hiyo hata kama yakitokea Mafuriko au ugonjwa kama huu wa Corona wananchi wote tupande ndege zetu tukakae angani.
Maendeleo hayana vyama.
Sent using Jamii Forums mobile app