"Makonda +Wadau wengine wa Taifa stars + Taifa stars+ maombi ya watanzania wengine wazalendo = Taifa stars 1,Harambee stars 0"

"Makonda +Wadau wengine wa Taifa stars + Taifa stars+ maombi ya watanzania wengine wazalendo = Taifa stars 1,Harambee stars 0"

Vision 2030

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2017
Posts
407
Reaction score
250
1.Mfumo wetu wa elimu hauturuhusu kukosea.

2.Anayepata A nyingi darasani ndio anayebebwa na mfumo,anayepata B mfumo unambeba mpaka anayepata C pia.

3.Tuliosoma bila vikwazo mpaka tunafika vyuo vikuu kwa kufuata mfumo huu mtakubaliana na Mimi.

4.Kundi kubwa ambao Mara nyingi ndio wanafanya vizuri,wapo nje ya mfumo nilioueleza hapo juu.

5.Uhalisia wa maisha ni kwamba ili ufanye vizuri katika maisha unahitaji ufanye makosa mengi ujifunze ili usonge mbele.Taa ya umeme iliwaka baada ya mgunduzi kufanya makosa 1013,Mara ya 1014 ndio taa iliwaka na Leo tunafurahia umeme.

6.Makonda ni kiongozi kijana ana mengi ya kujifunza na katika kujifunza kwake kuna maeneo anakosea na ndio ubinadamu wenyewe.

7.Sijaandika kumtetea Makonda,lakini cwezi kumpinga mtanzania mwenzangu katika kila kitu hata ambacho kinamaslahi kwa Taifa.

8.Makonda yupo Misri kuhamasisha Taiga stars ishinde ilete Heshima kwa nchi yetu kama ambavyo watanzania wengi tunatamani iwe.

9.Hili ni Jema hata kama unamchukia makonda personally au Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam.

10.Nina maana kwamba lile lenye maslahi kwa Taifa tuungane hata kama ni wanasimba au wanayanga,wanaazamu,wanalipuli n.k

11.Tuungane hata kama wanachadema/wana ccm/wana act-wazalendo

12.Tuungane waislam kwa wakristo kwa wapagani.

13.Hii ndio nchi yetu ,tunapoiwakilisha nchi yetu vizuri,ni sisi wenyewe tunanufaika na vizazi vyetu.

14.Nimalizie kwa kusema,kama watanzania leo tunahitaji kuwa wamoja na kuungana na wote tuliowatuma Misri kutuwakilisha wafanye vizuri,tuwaombee dua na kila jema wafanye vizuri.

15.Makonda nikuombe huko uliko wasisitize wachezaji sisi tunataka ushindi,hata kufungia mgongo inaruhusiwa.

"MUNGU IBARIKI TAIFA STARZ
MUNGU TUBARIKI WATANZANIA"
 
Harambee stars funga hao ccm stars waje waimbe nyimbo za kuunga juhudi. Hiyo timu imeshashikwa na wazandiki, hivyo ni bora ifungwe tu. Hata waganda waliowaunga mkono wanajeshi wa Tanzania kisa walikuwa hawamtaki Amini, ila ilikuwa haimaanishi kwamba hawaipendi Uganda.
 
Harambee stars funga hao ccm stars waje waimbe nyimbo za kuunga juhudi. Hiyo timu imeshashikwa na wazandiki, hivyo ni bora ifungwe tu. Hata waganda waliowaunga mkono wanajeshi wa Tanzania kisa walikuwa hawamtaki Amini, ila ilikuwa haimaanishi kwamba hawaipendi Uganda.
"Wewe hauwezi kuwa Mtanzania"
 
Najiandaa hapa kwenda kupata burudani kwa dogo Diatta kwanza kabla nawasubiri wendawazimu wakavyonyoshwa na Vijana wa Kenyata.


Uganda Mungu anawaona, mlituacha tufike AFCON halafu tukapambane na wendawazimu wetu huku ninyi mkiendelea kusonga mbele....
 
Back
Top Bottom