Dunia inao wachache mno wenye haki, na watenda maovu hujivuna kwa uovu wao, huutetea uovu wao, wako tayati kumwaga damu nyingine kutetea ujangili wao
Na siku zote mtu muoga wa kusemwa kwa sababu anasimamia ukweli, hawezi kuwatetea watu hadharani, mtu huyo huchagua njia ya kuabudu uovu na hayuko tayari kuitetea haki, maana haki haipendwi na wengi, Haki ni adui mkubwa sana ya watu wengi waovu
Na ndiyo maana leo, tunaviongozi wengi wanaabudu uovu wa matendo ya watishao kwa uovu wao, hawana kauli yoyote mbele ya watishao kwa maovu
Kuna kiongozi mmoja alidiriki kusema, ukiwagusa mafisadi, unaua nchi, hiyo ni ibada kamili ya mtu muovu dhidi ya waovu wenzake
Siku zote dhambi kuu, hubebwa na mabwenyenye yaliyoshindikana kwa uovu, yamejaa dhuluma na hayana hofu dhidi maisha ya haki na watu wengine, yana ukwasi na yanatisha, hayo hayawezi kukemewa hata kwenye nyumba za Ibada, lakini ni kwa faida ya Nani?
Ni kwa faida ya njaa tu za viongozi, wakati wao wakiamini wanamtumikia huyo mwenye haki, naye huyo mwenye haki hawaju hao, amewajumlisha kwenye kundi la hao waovu
Ushetani kuugeuza uwe wema, ni gharama kubwa mno, ni nani awezaye kuvumilia matusi ya waovu? Nani awezaye kutengwa? Kunyanyapaliwa na watu mamia na maelufu ya waovu? Mtenda haki, huwa kama mtu akaaye nyikani, maana hutengwa na kupigwa vita na jamii kubwa ya waovu
Duniani, tunaishi kwa muda mufupi mno ukilinganisha na Dunia tuliyotokea kabla ya kuja Duniani na baada ya kutoka tena tena Duniani
Chukia uovu kwa nguvu zote ili uwe mingoni mwa wale wanao na matumiani ya amani kutumika bila dhuluma huku wakijua, kufanya hivyo, ni kuwa upande wa wale wachache mno walio na tunda la Mungu ndani yao
Makonda, endele hivyo hivyo, hata kama heshima yako itakuwa ziro kabisa duniani, ila kwa kuwa unajipambanua kwa kuchukia dhuluma, Mungu anathawabu yako