MAKONDAKTA BHANA!

MAKONDAKTA BHANA!

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Daladala Ni Usafiri Nnao Tumia Kila Siku Kwenda Kwenye Mihangaiko Yangu. Basi Huwa Nakumbana Na Matusi, Dharau Na Kejeri Toka Kwa Baadhi Ya Makonda Wa Daladala. Hasa Pale Mkipishana Kauli Iwe Nauli Pungufu Au Kulipia Mzigo.

Yalinikuta Siku Moja Nikiwa Ndani Ya Daladala. Nakumbuka Nilitoka Sokoni Kununua Mahitaji Ya Gheto. Huwa Na Tabia Ya kununua Vitu Kwa Jumla Ili Nitumie Kwa Mwezi Mzima. Basi Siku Ile Nkapanga Bajeti Zangu Vizuri Nkatoka Gheto Nkiwa Na Hela ya Mahitaji Muhimu Na Nauli Ya Kwenda Na Kurudi Sokoni Tu.

Sikutaka Kutembea Na Pesa Za Ziada Kwani Zingesababisha Nizitumie Pasipo Ulazima.Nilipomaliza Kununua Mahitaji Sokoni Haraka Nikajitwisha Mzigo Wangu Begani. Nikawahi Standi Huku Mfukoni Nimebakiwa Na Mia Tano 500 Tu Ya Nauli. Stendi Nkapokelewa Na Mpiga Debe Nkahakikisha Kaweka Mzigo Kwenye Buti. Kisha Nkawahi Siti Ndani Ya Daladala.

Gari Ilipojaa Na Kuanza Kuondoka Konda Akauliza Mzigo Ni Wa Nani Kwenye Buti?. Nikamjibu Ni Wangu, Akasema Nimwandalie Nauli Ya Mzigo. Ukatokea Ubishani Wa Hapa Na Pale, Mimi Niking'ang'ania Kuwa Siwezi Kuulipia Mzigo Ule Ni Kidogo. Konda Akanambia Utalipia Tu, Ukishindwa Utaufata Polisi.

Konda Aliniwashia Moto Mpaka Akaingizia Maisha Yake Kwenye Majibizano. Mara Akasema Nisimuone Ni Konda Nikamdharau. Amesoma Chuo Na Ana Digrii Yake Katundika Tu Ndani Kutokana na Ukosefu Wa Ajira. Sheria Anazifahamu Hivyo Nisipolipa Ntakiona Cha Moto.

Niliishiwa Pozi Ndani ya Daladala Ile Nakumbuka Mmoja Kati Ya Abiria Akamwambia Konda. Muache Kwanza Atakaposhuka Ndo Atakuelewa Kuwa Upo Kazini.Nikatulia Kimya Tu Huku Nikitafakari Ntalimalizaje Suala Lile.

Tulipofika Stendi Konda Akaniambia Kama Sina Nauli Ya Mzigo.Twende Kwenye Kituo Cha Polisi Kilichopo Stendi Pale Tukayamalize. Sikubishaa Kwa Maana Sikuwa Na Pesa Ya Ziada Mfukoni.

Tulipofika Kwa Askari Alisikiliza Maelezo Ya Upande Wa Kondakta Tu, Aliyeonekana Kupaniki Kupita Kiasi.Askari Akaamuru Nilipie Mzigo Kama Sina Pesa Nikatafute. Nije Kulipa Maana Mzigo Upo Kwenye Mikono Salama.

Basi Nami Nikachafukwa Kichaa Cha Kutafuta Maisha Kikanipanda. Nkamwambia Yule Askari Kuwa Wewe ni Msomi Na Utakuwa Unazijua Sheria Za Usafirishaji Vizuri. Na Hata Konda Nae Ana Digirii Yake Nyumbani.

Nkawaambia Wote Kwa Pamoja Wanisikilize Vizuri. Sheria Za Sumatra Zinasema Kila Kilometa Moja Napaswa Kulipa Shilingi Arobaini na Mbili 42. Kutoka Sokoni Mpaka Hapa Ni Kilometa Kumi 10. Hivyo Ukipiga Hesabu 42×10=420! Lakini Mimi Nimetozwa Shilingi Mia Tano 500.Tayari Nimezulumiwa Shilingi Themanini 80 Hapo. Pili Sheria Ya Mizigo Inasema Mzigo Kuanzia Kilo Ishirini 20 Ndiyo Utalipiwa Nauli Ndani Ya Gari La Abiria.

Nkahitimisha Kwa Kusema Tupime Mzigo Huo Kama Utakuwa Na Kilo Ishirini 20.Ntaulipia Hapa hapa Kinyume Na Hapo Sheria Ifate Mkondo Wake.Basi Yule Konda Akiwa Bado Kapaniki Akamwita Kijana Wa Mzani. Tukapima Mzigo Ukakutwa na Kilo Kumi Na Sita 16 Tu.

Basi Askari Akamuru Niende Zangu.Nkatoka Nikiwa Natabasamu Huku Konda Akiwa Kafurika Hasira.Akaniangalia Kwa Jicho Kali la Hasira. Nkamwambia Pole Kaka Siku Nyingine Uwe Unatembea Na Digirii Yako! [emoji1787]

Positive Mind Is Better Than Knowledge! [emoji123]

[emoji1241]
FB_IMG_1564594788552.jpeg
 
[emoji1241]View attachment 1168699
Hahahahahhahhahh!!!!!!! Nimeipenda hii story na nimejifunza kitu pia kupitia kwako ,God bless you [emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
 
muda huo wote ad kupelekana polisi inaweza kuwa mtoa mada alidaiwa jero ya mzigo
 
Back
Top Bottom