Makongoro Nyerere aunganishwa kwenye kesi ya Abubakar Marijani “Papaa Msofe”

Shadow

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2008
Posts
2,897
Reaction score
675
[TABLE="width: 1696"]
[TR]
[TD][h=2]

Makongoro Nyerere aunganishwa kwenye kesi ya Abubakar Marijani “Papaa Msofe”
[/h][COLOR=#333333 !important][FONT=Georgia !important]13/02/2013[/FONT][/COLOR]
[COLOR=#333333 !important][FONT=Georgia !important]0 Comments[/FONT][/COLOR]


[COLOR=#333333 !important][FONT=Georgia !important]Imeandikwa na Happiness Katabazi, Dar es Salaam via blog --


MFANYABISHARAmwingine na Mkazi wa Pugu jijini Dar es Salaam, Makongoro Joseph Nyerere jana aliunganishwa kati kesi ya mauji inayomkabili mfanyabishara maarufu jijini hapa Abubakar Marijan [50] maarufu kwa jijini ‘Papaa Msofe chuma cha Reli akishiki Kutu mutu ya Pakee’.

Nyerere alifikishwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na askari kanzu na kabla ya wakili wa serikali Charles Anindo kuanza kumsomea mashtaka , wakili huyo aliomba ruhusa ya mahakama ili aweze kubadilisha hati ya mashtaka, ya awali iliyokuwa ikimhusu mshtakiwa mmoja tu Papa Msofe, ili mshtakiwa huyo Nyerere awe kuunganishwa katika kesi hiyo ya mauji.

Hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo Agnes Mchome alikubaliana na ombi hilo la upande wa jamhuri , lakini akamtaka mshtakiwa huyo kuwa haruhusiwi kujibu chochote baada ya kusomewa shitaka linalomkabili kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba ni mahakama kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili Anindo akimsoma shtaka alidai kuwa baada ya mahakama hiyo kukubali ombi lake la kuifanyia marekebisho hati hiyo ya mashitaka ambayo awali ilikuwa ikisomeka ni ya mshitakiwa mmoja tu(Papa Msofe), hivyo kuanzia jana kesi hiyo itasomeka kuwa inawakabiliwa washitakiwa wawili ambapo mshitakiwa wa kwanza ni Papa Msofe na Nyerere ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Pugu jijini Dar es Salaam.

Wakili Anindo alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kumua kwa makusudi Onesphory Kituli, kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu sura ya 19 kama kilivyorekebishwa mwaka 2002 na kwamba kosa hilo walilitenda Oktoba 11 mwaka 2011, nyumbani kwa marehemu huko Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka hilo, Hakimu Mchome aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 20 mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa na akaamuru Nyerere apelekwe gerezani kwasababu kosa analokabiliwa nalo yeye na mwenzi Papa Msofe ambaye tayari yupo gerezani tangu Agosti 10 mwaka jana, halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Agosti 10 mwaka jana , Papa Msofe alipandishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza chini ya ulinzi mkali wa askari polisi na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mchome alidai mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa hilo la mauji[/FONT][/COLOR]​




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Source: Makongoro Nyerere aunganishwa kwenye kesi ya Abubakar Marijani
 
Hizi habari za kuuzia magazeti hatari kweli! Eti Makongoro Nyarere!

Acheni upuuzi bwana, watu tumefungua tunafikri yule tunayemfahamu kumbe kinyamkela sijui cha wapi? Mwandishi huyu bure kabisa. Kwa nini asitofautishe kati ya Makongoro wa Mwalimu na Makongoro wa mdogo wa mwalimu (kama ni hivyo kweli?)
 
Papaa Msofe ameenda jumla na vijana wake...watu watanashati...hawaonekani kabisa ndio maana mzunguko wa hela umepungua. Teh teh teh
 
Nilifikiri yule jirani yangu kumbe Makongolo mwengine
 
Wee Angle maskini anko nini, kwani hujui yakua mshahara dhambi ni mauti isome iyo sasa...!
 


Eti amebadilishiwa Mashitaka. Je kuna uhusiano na hatua ya Ugombea wa wanafamilia wa jina la Nyerere?



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…