Makosa 4 aliyoyafanya Harmonize mpaka sasa

music mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
485
Reaction score
876
1: Kuruhusu upande wa WCB kutangulia kueleza tofauti yao.

Baada ya Salam SK, kuongea, asilimia kubwa imeshaamini kua Harmo anaondoka WCB kwa jeuri. Kiburi, kujisikia na amekosa fadhila. Itamchukua muda sana kulifuta hili kwenye safari yake. Ukweli hua hauzungumzwi mara mbili.

2: Kumfolow Ali Kiba.
Bila shaka kichwani Harmonize anawaza ukubwa wake utakavyokua baada ya kuondoka WCB. Kwa vyovyote vile ili aupate ukubwa huo ni lazima apambane kusimama juu ya au kufika pale walipo Kiba na Diamond

Kufika hapo si kwa idadi ya watu wanaosikiliza ngoma zako ila ni kua na idadi kubwa ya watu wako wanaokuamini. Wasanii wengi wameua carear zao kwa kukosa uvumilivu wa kutengeneza mashabiki wao, wengi wamenasa kwenye mtego wa Kiba na Mondi. Ref Baraka da Prince, Rich Mavoko.

Kumfolow Kiba sasa ni ishara ya kutafuta huruma ya upande wa pili. Upande ambao unapambana na upande wa Diamond. Huku anaweza kupata nusu watakaomsapoti lakini lazima ajue kwa upande wa mashabiki wa WCB hakuna atakaemsapoti tena. Ameiweka rehani biashara yake!

3: Kujaribu kuacha 'kivuli chake WCB.' .
.
Ni vyema kuonekana bado anaipenda WCB, lakini kwa faida ya kazi yake na aina ya mashabiki tulionao, Harmo hatakiwi kuihusisha kazi yake na WCB. Kufanya hivyo huenda hili likawa kaburi lake kimuziki.

Kuna dhana ya unafki itaanza kumtafuna. Kama alifuta ile kusainiwa WCB, hakukuwa na ulazima wa kuacha neno WCB for Life kwenye Bio yake. Kwa lugha ya Salam SK, Harmo alianza kuivimvimbia menegament yake kabla ya kutoka. Hakuna anayejua nyuma ya kicheko cha Diamond, kuna nini.
.
.
4: Kutaka kuachia wimbo mpya haraka
Hili ni kosa kubwa sana. Saa chache baada ya Salam SK kuongea, Harmo amepost cover kua yuko mbioni kuachia ngoma. Hii ni tension mbaya sana anaitengeneza.
Kwa sababu ya presha ya hivi sasa, wako watakaoichukia kazi yake. Haijalishi ubora wake, Liko sikio litamkataa tu kwa kuonekana ana kiburi cha kushindana.

Iko dhana ya 'KIKI' pia inaweza kuingia. Akaonekana mtu wa drama za mitandao. Hii ni mbaya sana.

NB: Pengine Harmo hajajua kua ni ngumu kuitofautisha WCB na Diamond. Ajipange kwa yote.
 
Ngoja nikusahihishe hiyo no 1 naona km vile ujaisikia interview ya sallam hakuna sehemu uongozi wa wcb uliomsema vibaya harmo Wala harmo kaisema vibaya Bali wamekubaliana pande zote mbili kukubali kuuvunja mkataba na pia uongozi wa wasafi wamempa baraka zote harmo na wamemuambia Kama atashindwa kujisimamia anaruhusiwa kurudi kwenye label au Kama anaitaji sapoti ya wcb watampa ila nimeona Kama mashabiki wa wasafi ndo wenye kinyongo kwa harmo.
 
Ufipa wamehamia kupinga kila kitu kuhusu muziki [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tokea nikujua humu JF Leo ndo nimeona uki andika kitu Kisicho cha kishabiki✅✅✅
 
Uwe unaandika na jina la mahali ulipoitoa hiyo habari
 
Kwanini mnachukulia haya mambo kwa mtazamo wa chuki aisee. Kwani akim follow Ali Kiba wewe mkuu ukiwa kama mshabiki wa Diamond unapoteza nini. Kwani ugomvi asee.

Si mumuache jamani, kama anakosea au anapatia si ni yeye na maisha yake. Boss hangaika na yako ugali uende kinywani, mambo magumu sasa hivi kuanza kumfatilia mtu unapoteza timing ya kulenga ili ya kwako yaende!

Ni kama mashabiki wa Diamond mmeachwa na mshangao sana na hamuamini kabisa kuwa huyu dogo kajitoa kwenye lebo.
 
Vyote amefanya kwa usahihi na hekima
1. Kuacha management iongee ni hekima kubwa kuliko kuanza kuisema vibaya au kusema vibaya ulipotoka
2. Kumfollow Alikiba pia ni jambo la busara maana hawezi endelea kuwa na beef ambalo hajui chanzo chake hata kwenye msiba wa Ruge alienda toa pole japo hajawahi kusimamiwa nae
3. Kwa nini ajionyeshe kinafiki bado anaipenda? Kuandika tu WCB for life ni heshima kubwa sana ameipa nashan pia anatatoo ya aliekua boss wake.
4. Kwa nin andelee kushikiliwa akili na mtu hata wakati akiwa huru? wimbo anatakiwa kuachia kulingana na ratiba zake za kibiashara ambapo anajua atatengeneza pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…