Makosa aliyoyafanya Humphrey Polepole yasijirudie tena na wengine walioasisi nafasi yake

Makosa aliyoyafanya Humphrey Polepole yasijirudie tena na wengine walioasisi nafasi yake

Brightg

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
372
Reaction score
662
Humphrey Polepole alifanya kazi nzuri sana ila alipokosea ni pale alipotaka kuonyesha kuwa kazi yake kwenye chama ni kubwa na ana uwezo mkubwa wa kukifikisha chama sehem ya juu, alitoa wazo ambalo viongozi wake wa juu ukimtoa mwenyekiti wake wa chama hakushirikishwa, hao viongozi wake wa juu walimuachia mpini ili aunge shoka na aingie kupasua kuni ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na wakurugenzi wa miji na kuwa kitu kimoja kwa kauli moja ya utekelezaji wa USHINDI WA KISHINDO.

Huu ushindi umeonekana utakipa chama tawala muda mgumu sana na mwenyekiti wao kuongoza maana hata 50% ya wananchi kushiriki maendeleo ya nchi inaweza ikawa ni ngumu sana sana, ushirikishwaji na ushiriki wa wananchi una misingi yake na una matunda yake (ujenzi wa madarasa hadi sasa hakuna mwenyekiti wa mtaa/kijiji, mbunge, mkuu wa wilaya aliye jitokeza kuhubiri sera hii kwa wananchi ili wajitokeze kwa wingi kuchangia).

Kwa sasa ni nani kiongozi wa kisiasa atakaye simama na kuzungukia wananchi kuwahamasisha kuhusu kuchangia maendeleo yao. wangapi watashiriki, haya ni maswali lazima tujiulize na tupate majibu.

Humphrey Polepole alikuwa bado mdogo sana kuondolewa katika nafasi ile maana bado kijana anayeweza kukitumikia chama vizuri sana tu, kumuondoa kuliibua maswali mengi sana ukizingatia hajaomba kuondolewa pale, anajifariji ila ukweli ndio huo.
 
Afadhali yako wewe unamjua ni kijana, mimi nilishashindwa.

Kususia uchangiaji wa elimu ni kuwadumaza watoto wetu
 
sie tuko tushaanza likizo ya Christmas
Wishing you all a happy Christmas season and New year 2021
pine-trees-in-christmas-snow.jpg
 
Mgonjwa wa Viieite. Nafasi yake inaarudishwa ilikitoka. Atajua hajui
 
Mr. Humphrey unamsingizia tu. Hakuwa katibu wa uenezi wakati mheshimiwa mwenyekiti anakabidhiwa kigoda hicho kwa kishindo cha 100%. Yaliyojiri baada ya hapo inaweza kuwa ni muendelezo tu wa vishindo.
 
UCHAGUZI ULIKWISHA KITAMBO, SASA TUFANYE KAZI. MUACHE KIJANA ACHAPE KAZI. TUSONGE MBELE.
 
Back
Top Bottom