SoC02 Makosa gani 5 watu hufanya katika miaka yao ya 20's ambayo yanahakikisha kuwa watakuwa na maisha magumu

SoC02 Makosa gani 5 watu hufanya katika miaka yao ya 20's ambayo yanahakikisha kuwa watakuwa na maisha magumu

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 31, 2022
Posts
45
Reaction score
98
1. Kuingia kwenye uraibu
Madawa ya kulevya,ulevi,ngono,bangi na uvutaji wa sigara ni moja ya mashimo hatari yanayonasa vijana.Uraibu ni njia tu ya kufanya maisha kuwa magumu zaidi. Yatachukua muda wako,afya na umakini wako wote kutoka kwa mambo ambayo ni muhimu sana.

2. Kuiga tabia mbaya.
Kuiga kunaua ubunifu wako.Inakuacha mtupu na kuchanganyikiwa, ukishangaa wakati wako wote ulienda wapi.Wakati wenzako wa rika yako wakipiga hatua tabia hii itakuvuta nyuma.Mfano:Ufujaji wa pesa

3. Kutojitolea kwa kitu chochote
Kutoanza mapema kujitolea ili kupata ujuzi au ufundi fulani ni pigo kubwa kwa vijana.Maisha ya kawaida yamejaa matokeo ya kawaida. Usipojifunza kujitoa na kutoa 100% ya muda wako kwa ajili ya ishu fulani ya faida au uzoefu , utaishia kuwa mtu wa wastani.

4. Kukosa kujidhibiti
Vijana wengi hawawezi kujidhibiti hasa kihisia.Hili linapelekea kupata mimba/ kufungwa jela/kuachishwa masomo/kufariki(ajali)na hatimaye maisha kuharibika.


5. Kutokujiamini
Maisha yamejaa changamoto, kushindwa na mashaka. Imani yako ndani yako itajaribiwa mara kadhaa. Ikiwa huna imani thabiti ndani yako, utaanguka.

6. Kutojifunza kwa waliokuzidi
Kudharau na kupuuza mashauri ya wakubwa zako hasa wazazi na walezi hufanya mwanguko ya maisha.Ukosefu wa utii wa wa wazee kunasababisha maisha ya vijana wengi wa 20's kuwa magumu baadae.

7. Kutokujiwekeza kiujuzi na kielimu
Ujuzi na ufundi haiozi Kokosa Ujuzi/elimu au ufundi katika umri mdogo kutokufanya ujutie baadae.
Ndio maana maneno ya vitabu vya dini vinahimiza.,Mshike sana elimu USIMUACHE aende zake.Elimu ni mtu,anashikika,anaongea,anafundisha, anaweza kukusaidia kwenye maisha.

Endelea kujifunza.
Unaweza kuorodhesha zaidi mambo ambayo vijana wa miaka ya 20's wanayafanya ambayo huwagharimu.

Kura yako ni muhimu.
Asante.
 
Upvote 7
Vjlxu
giphy.gif
 
Back
Top Bottom