Makosa katika rambirambi za kifo cha Kleist Abdulwahid Sykes TBC

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
upload_2017-11-24_23-54-52.png

Ndugu zanguni mimi nimeangalia TBC taarifa ya habari ya jana
usiku tarehe 23 Novemba siku aliyozikwa Kleist Sykes.

Rambirambi zilikuwa na makosa.

Mtangazaji anampa Kleist sifa za kuasisi African Association 1929
sifa ambayo ni ya babu yake jina lake Kleist Sykes Mbuwane.

Kisha mtangazaji anampa Kleist sifa ya kuasisi TANU 1954 na
kupigania uhuru wa Tanganyika ambayo ni sifa ya baba yake
Abdulwahid Kleist Sykes.
 
Aiseeeee

Inabidi wajitafakari na kuacha kukurupuka bila kukimbilia kutangaza tu.
 
Lakini yote kwa yote at least itifaki imezingatiwa....wangekaa kimya humu siyo hizo thread za malalamiko basi mpaka wengine wasingepata nafasi ya kupost chochote.Mungu aipokee roho ya marehem aipe pumziko jema amina.
 
Ni tatizo kubwa kweli kweli kila siku yanajirudia sio tu TBC bali vyombo vingi vya habari hapa Tanzania. Mwandishi hawezi hata kuandika makala ya uchambuzi, kutafuta vyanzo tafauti vya habari. Mwandishi mwenye ueledi na maarifa angetengeneza documentary fupi tu ya kueleza ni nani huyu Kleist A. Sykes lakini ndo hivyo tena hakuna hata mmoja, wengi wao wamezoea habari za "bigijii", leo daraja jipya lafunguliwa, kesho Waziri mkuu kuzuru Serengeti ambazo zitaandikwa na kutangazwa na kila chombo cha habari na "yellow journalism" pia.
 
View attachment 637456

Ndugu zanguni mimi nimeangalia TBC taarifa ya habari ya jana
usiku tarehe 23 Novemba siku aliyozikwa Kleist Sykes.

Rambirambi zilikuwa na makosa.

Mtangazaji anampa Kleist sifa za kuasisi African Association 1929
sifa ambayo ni ya babu yake jina lake Kleist Sykes Mbuwane.

Kisha mtangazaji anampa Kleist sifa ya kuasisi TANU 1954 na
kupigania uhuru wa Tanganyika ambayo ni sifa ya baba yake
Abdulwahid Kleist Sykes.
ASsalaam Aalaykm wa RahmatuLLAHI wa Berakatuh.
INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAJIU'UN.
ALLAH SUBHANA WA TAALA AMGHUFURIYE ZHAMBI ZAKE NA AMREHEM. AAMIYN

Naona wana maanisha ya kwamba familia hii ya Senior Kleist Sykes mpaka kumfikia huyu Marhem wameitumikia nchi yetu kwa Hali na mali na uzalendo wa hali ya juu. AlHmduliLLAHI.
 
Knowledge...
Haya hapo chini niliyaandika hapa JF hebu pitia kuna kitu utakiona:
''Kolorama,
Umesema kweli kufutwa kwa majina katika historia ya TANU na
uhuru wa Tanganyika hakukuwa kwa bahati mbaya.

Lile jopo la waandishi wa Chuo Cha Kivukoni walikuwa wanafata
maelekezo waliyopewa vipi waandike historia ile.

Swali la kwanza la kuuliza ni nani huyu aliyetoa maelekezo ya vipi
historia ya TANU iandikwe?

Bila shaka atakuwa kiongozi mwenye nguvu sana ndani na nje ya
chama.

Katika jopo lile nilikuja kujuana na wajumbe wawili na wote makada.
Dr. Mayanja Kiwanuka na Hassan Upeka.

Hassan Upeka ni marehemu.

Huyu ni mtu wa Dar es Salaam na ni mtumishi wa kwanza kuajiriwa
na TANU 1956 alipomaliza darasa la 10 Tabora School.

Upeka alikuwa kachero wa TANU kastaafu miaka ya 1980 akiwa katika
kazi hiyo.

Hakuna kijana wa Dar es Salaam wa umri wangu aliyekuwa hamjui kaka
Upeka kwani akiogopewa kwa ile kazi yake.

Lakini hakupata kumnyayanyasa mtu yoyote kwa wadhifa wake ila nasikia
mara moja moja alikuwa akipita Mnazi Mmoja kuwatisha wauza bangi na
kuwaambia atawaletea polisi ikiwa wataendelea na kazi hiyo.

Vinginevyo alikuwa mtu mtaratibu na mkimya sana.
Labda ni kutokana na mafunzo ya kazi yake.

Upeka akinijua kama bwana mdogo tu lakini alipostaafu tukawa karibu sana.
Wakati huo mimi nishafanya mhadhara wangu wa kwanza Mnazi Mmoja na
kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru nikidai wazee wetu
wapewe heshima wanayostahili.

Cassette za mhadhara huu ziliuzwa kama maandazi ya moto.
Kila kibanda cha kuuza inawekwa na watu wamejazana wananisikiliza.

Kipindi hiki nishaandika ile makala ambayo gazeti zima lilikusanywa na
kutolewa katika mzunguko kwa sababu nilimtaja Abdul Sykes kuwa muasisi
wa TANU.

Hili lilikuwa Africa Events likichapwa London.

Makala zangu kuanzia 1990 zikawa maarufu na zikivutia wasomaji wengi.
Africa Events na New African yote magazeti ya London yakinichapa.

Katika hali hii siku moja Upeka aliniomba nende tukae faragha ofisini kwake.
Ofisi yake ilikuwa Mtaa wa Mvita, Karikaoo.

Upeka alinifungulia kifua chake kuhusu tatizo alilokutananalo wakati wa
kuandika historia ya TANU.

Akanieleza pia jinsi alivyomsaidia John Iliffe wakati ule mwalimu wa historia
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kupata nyaraka za TAA na TANU zilizokuwa
TANU Office, Lumumba Street.

Akanieleza pia kuhusu ''notes,'' za Abdul Sykes alizoandika katika mazungumzo
na yeye kuhusu historia ya TANU.

Upeka akanambia kuwa ''notes,'' hizi zilikataliwa na jopo.
Jopo liliamua kuandika historia ya TANU bila kumtaja Abdul Sykes.''

Knowledge,
Laiti Chuo Cha Kivukoni ingeliandika historia ya TANU inavyostahili hapengekuwa
hii leo na tatizo la kutoijua historia yetu wenyewe.
 
Lakini yote kwa yote at least itifaki imezingatiwa....wangekaa kimya humu siyo hizo thread za malalamiko basi mpaka wengine wasingepata nafasi ya kupost chochote.Mungu aipokee roho ya marehem aipe pumziko jema amina.
 
Waislamu awamu hii ndio msahau kabisa, JK alipigwa sana vita kwa sababu ya dini yake.

Leo mwanaparokia mwenzetu yupo magogoni Taifa zima linalazimishwa kuimbishwa singeli ya uzalendo, na hata hii thread yako utaitwa mchochezi na umekosa uzalendo.

Nilikuwa napuuza sana malalamiko ya waislamu lakini kwa sasa naona waziwazi hasa baada ya mpaka mzizima inatawaliwa na mshamba.

Hapa ndipo sera ya majimbo ya Chadema naiona mantiki yake, ni makosa kwa mshamba kitoka usukumani kuja kututawala wana Mzizima.
 
Knowledge...
Haya hapo chini niliyaandika hapa JF hebu pitia kuna kitu utakiona:
''Kolorama,
Umesema kweli kufutwa kwa majina katika historia ya TANU na
uhuru wa Tanganyika hakukuwa kwa bahati mbaya.

Lile jopo la waandishi wa Chuo Cha Kivukoni walikuwa wanafata
maelekezo waliyopewa vipi waandike historia ile.

Swali la kwanza la kuuliza ni nani huyu aliyetoa maelekezo ya vipi
historia ya TANU iandikwe?

Bila shaka atakuwa kiongozi mwenye nguvu sana ndani na nje ya
chama.

Katika jopo lile nilikuja kujuana na wajumbe wawili na wote makada.
Dr. Mayanja Kiwanuka na Hassan Upeka.

Hassan Upeka ni marehemu.

Huyu ni mtu wa Dar es Salaam na ni mtumishi wa kwanza kuajiriwa
na TANU 1956 alipomaliza darasa la 10 Tabora School.

Upeka alikuwa kachero wa TANU kastaafu miaka ya 1980 akiwa katika
kazi hiyo.

Hakuna kijana wa Dar es Salaam wa umri wangu aliyekuwa hamjui kaka
Upeka kwani akiogopewa kwa ile kazi yake.

Lakini hakupata kumnyayanyasa mtu yoyote kwa wadhifa wake ila nasikia
mara moja moja alikuwa akipita Mnazi Mmoja kuwatisha wauza bangi na
kuwaambia atawaletea polisi ikiwa wataendelea na kazi hiyo.

Vinginevyo alikuwa mtu mtaratibu na mkimya sana.
Labda ni kutokana na mafunzo ya kazi yake.

Upeka akinijua kama bwana mdogo tu lakini alipostaafu tukawa karibu sana.
Wakati huo mimi nishafanya mhadhara wangu wa kwanza Mnazi Mmoja na
kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru nikidai wazee wetu
wapewe heshima wanayostahili.

Cassette za mhadhara huu ziliuzwa kama maandazi ya moto.
Kila kibanda cha kuuza inawekwa na watu wamejazana wananisikiliza.

Kipindi hiki nishaandika ile makala ambayo gazeti zima lilikusanywa na
kutolewa katika mzunguko kwa sababu nilimtaja Abdul Sykes kuwa muasisi
wa TANU.

Hili lilikuwa Africa Events likichapwa London.

Makala zangu kuanzia 1990 zikawa maarufu na zikivutia wasomaji wengi.
Africa Events na New African yote magazeti ya London yakinichapa.

Katika hali hii siku moja Upeka aliniomba nende tukae faragha ofisini kwake.
Ofisi yake ilikuwa Mtaa wa Mvita, Karikaoo.

Upeka alinifungulia kifua chake kuhusu tatizo alilokutananalo wakati wa
kuandika historia ya TANU.

Akanieleza pia jinsi alivyomsaidia John Iliffe wakati ule mwalimu wa historia
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kupata nyaraka za TAA na TANU zilizokuwa
TANU Office, Lumumba Street.

Akanieleza pia kuhusu ''notes,'' za Abdul Sykes alizoandika katika mazungumzo
na yeye kuhusu historia ya TANU.

Upeka akanambia kuwa ''notes,'' hizi zilikataliwa na jopo.
Jopo liliamua kuandika historia ya TANU bila kumtaja Abdul Sykes.''

Knowledge,
Laiti Chuo Cha Kivukoni ingeliandika historia ya TANU inavyostahili hapengekuwa
hii leo na tatizo la kutoijua historia yetu wenyewe.
Mwenye-Enzi-Mungu-Allah-Mlezi Amlaze pahala pazuri our dear brother Junior Kleist Sykes. Aamiyn
 
Wanahabari wetu wanamapungufu sana,hawtaki kujua vitu kwa undani kabla ya kuviweka hadharani. Nimekuwa nashangazwa hata kutamka baadhi ya majina ya viongozi au watu maarufu duniani unakuta mwanahabari anatamka ndivo sivyo unajiuliza kwanini hawakai wakajifuza aidha kwa kuangalia habari za dunia kutoka vyombo vya habari vya nje. Kwa kweli ni aibu.
 
ASsalaam Aalaykm wa RahmatuLLAHI wa Berakatuh.
INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAJIU'UN.
ALLAH SUBHANA WA TAALA AMGHUFURIYE ZHAMBI ZAKE NA AMREHEM. AAMIYN

Naona wana maanisha ya kwamba familia hii ya Senior Kleist Sykes mpaka kumfikia huyu Marhem wameitumikia nchi yetu kwa Hali na mali na uzalendo wa hali ya juu. AlHmduliLLAHI.
 
View attachment 637456

Ndugu zanguni mimi nimeangalia TBC taarifa ya habari ya jana
usiku tarehe 23 Novemba siku aliyozikwa Kleist Sykes.

Rambirambi zilikuwa na makosa.

Mtangazaji anampa Kleist sifa za kuasisi African Association 1929
sifa ambayo ni ya babu yake jina lake Kleist Sykes Mbuwane.

Kisha mtangazaji anampa Kleist sifa ya kuasisi TANU 1954 na
kupigania uhuru wa Tanganyika ambayo ni sifa ya baba yake
Abdulwahid Kleist Sykes.
Mkuu,mwalimu wangu hawa watu hakuna walijualo,wanafanyakazi kwa mtindo wa watssup.
 
Back
Top Bottom