mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Kutokana na ushauri wa kuvaa barakoa kama njia mojawapo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya kirusi cha korona wengi wetu wanafanya makosa yafuatayo ya uvaaji wake.
1) Barakoa kufunika tu mdomo. Uwezekano wa kuambukizwa kupitia pua ni mkubwa ukivuta hewa yenye virusi. Hii ni pamoja na kuiteremsha chini ya kidevu wakati unapongea. Baadhi ya watu wakiongea mate pia humtoka, kama ameambukizwa atasambaza virusi.
2) Barakoa inagusana na mwili au mavazi yako, kama yatakuwa na virusi, wakati wa mishemishe za maisha na hasa utumiapo usafiri wa umma kugusana na watu hakuepukiki. Hivyo siyo salama kuigusagusa, mathalani kutaka kuirekebisha ikae vizuri usoni.
3) Barakoa inalegea usoni. Barakoa N95 zivaliwazo na watumishi wa afya zimetengenezwa kwa utaalamu kiasi cha kubana uso inavyostahili. Lakini barakoa zingine, hasa zinazoshonwa na mafundi mitaani, nyingi hazikai vizuri usoni na kuongeza uwezekano wa kupitisha makohozi au chafya zenye virusi iwapo aliyevaa atakuwa ameambuukizwa.
Pia kama ilivyoelezwa kwenye 2) itamlazimu mvaaji kuirekebisha mara kwa mara kiasi cha kuongeza uwezekano wa kujiambukiza. Isitoshe kama una ndevu nyingi, uwezekano wa barakoa kutokukaa vizuri usoni ni mkubwa. Hivyo wenye ndevu mnashauriwa kupunguza ndevu maana barakoa ukiivaa ndevu zitaivuta chini na kuacha pua imefunikwa nusu nusu.
4) Barakoa inafunika sehemu ndogo ya pua badala ya pua yote. Wakati wa kuvaa barakoa, hasa zenye chuma, ibane kwenye pua kwanza.
5) Barakoa siyo safi na salama kutumika. Kama unatamani kuitumia barakoa tena, hakikisha umeisafisha kwanza ama kuipiga pasi (zinazotengenezwa mitaani) au ya N95 kuitundika kwenye mvuke wa maji yanayochemka kwa dakika kama 15 na kisha kuanikwa ikauke ili isivaliwe ikiwa mbichi. Kamwe usiendelee kutumia barakoa iliiyochakaa au isiyo safi.
COVID-19 ni ugonjwa hatari ambao hauna chanjo wala tiba. Njia ya kuepukana na maambukizi ni yako mwenyewe kwa maamuzi yako binafsi kuzingatia au la, ushauri unaotolewa mara kwa mara na wataalamu wa afya na wewe mwenyewe kubadili tabia.