mzenjiboy
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 907
- 385
Nadhani kabla ya kutengeneza rasimu ya kwanza na ya pili na hatimae kupatikanwa kwa katiba mpya, kwanza kabisa kulikuwa na haja ya kupiga kura ya maoni juu ya muungano kama raia wa pande mbili wanautaka au hawautaki. Endapo kungepatikana majority kura ya NDIO hapo ndio pangelifanyika mchakato wa kupata katiba mpya. Na kungepatikana kura nyingi za HAPANA hapo tena kungelikuwa na maneno mengine. Ama kuweka kura ya maoni mwisho na ikiwa walio wengi wakikataa muungano ina maana mambo yote yaliokwisha kutekelezwa itakuwa ni bure pamoja tukizingatia na gharama zake. Kwa maoni yangu kilichotendeka ni makosa lakini ndio twendeni nalo.