Makosa ya dola katika kuteua wagombea viti maalumu?

Makosa ya dola katika kuteua wagombea viti maalumu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Tukubali kwamba nchi au wanamikakati wa siasa za Tanzania waliopo Sasa wamekosa mikakati.

Tukubali kwamba dola imekwama sehemu katika kuplan na kutekeleza mikakati yao.

Tukubali kwamba wasomi waliokabidhiwa dhamana ya kutuongoza ikiwemo tume imekosa uzalendo na kujisimamia.

Tukubali kwamba tumekuwa tunatumia nguvu na amri kwenye Mambo yanayohitaji mikakati.

Kwanini tumtoe mtu mahabusu usiku na asubuhi tumwapishe? Kwani tungemruhusu akawa uraiani kwa miezi kadhaa au siku kadhaa mkakati usingetimia?

Kwanini tume ivunje sheria waziwazi bila hata kificho? Kwanini Bunge liwe kijiwe Cha watu wachache kufanya wanavyoona inafaa? Kwanini vyombo hivi vinajidhalilisha?

Mnyika kwa press moja ya leo amevivua nguo vyombo hivi, chadema kila siku wamekuwa wakitumia madhaifu haya ya kimfumo kupata simpathy ya wananchi Jambo linalowaimarisha kila siku.

Dola mnakosaje strategists?
 
Bongo movie adi kwenye siasa....
sijui tutaendelea lin na hii tasnia...
 
Nchi inaendeshwa kwa amri ya mtu mmoja, tena siku hizi hata sheria hawafuati, wanafanya mambo yao hovyo kiholela sana wakidhani wanawakomoa wapinzani kumbe wanazidi kujishushia heshima zao.

Wanajiita "donor kantri" lakini ukiangalia kwa makini hicho walichokifanya ni kujaribu kuwadanganya mabeberu ili waendelee kupokea zile 1.6 trillion za kukuza demokrasia, ambazo kigezo cha kuzipata ilikuwa lazima wapinzani wawepo bungeni kuongoza zile kamati mbili (LAAC na PAC).
 
Tanzania hakuna wana harakati wala wapinzani, kuna waropokaji wajuaji wenye njaa, wakilushiwa fupa lazima wakimbilie, si Zitto, Lissu au Mbowe wote wana price tag.
 
Tanzania hakuna wana harakati wala wapinzani, kuna waropokaji wajuaji wenye njaa, wakilushiwa fupa lazima wakimbilie, si Zitto, Lissu au Mbowe wote wana price tag.
Meko ndio mropokaji na kilaza kama wewe dada yake
 
Tukubali kwamba nchi au wanamikakati wa siasa za Tanzania waliopo Sasa wamekosa mikakati...

Weee ndio huoni dola ilivyo na srategist wazuri....ha ha ha

Sasa huoni kama CCM wameingia wote bungeni na CDM wanatoa kambi ya upinzani bado wee unasema hawana wana mikakati?? Utakuwa fala

Unataka wana mikakati wafanye vitu vyote kwa sheria? Au kwa haki? Mambo mengine yanaenda kwa kuvunja sheria

Mtapiga kelele wiki moja mtasahau.

Siasa zitaendelea
 
Tukubali kwamba nchi au wanamikakati wa siasa za Tanzania waliopo Sasa wamekosa mikakati.

Tukubali kwamba dola imekwama sehemu katika kuplan na kutekeleza mikakati yao..
Wanajifanya kununua wanasiasa wasio na msimamo ili kuwarubuni wanaowaita mabeberu wasiwapige pini. Hawajui kuwa siasa za dunia hii zinatawaliwa na hao wanaowaita mabeberu na wanalolifanya wala sio jipya maana lilishawai kufanywa hapo Kongo tu na Mobutu Seseko
 
Back
Top Bottom