Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
MAKOSA YA JINAI CHINI YA SHERIA YA TAKWIMU.
Mr. George Francis.
0713736006
mr.georgefrancis21@gmail.com
Habari ndugu mtanzania,
Karibu tuwe pamoja katika kusoma na kufahamu makosa ya jinai chini ya Sheria ya Takwimu ili usije ukaingia hatiani na kukumbana na adhabu kali katika zoezi la ukusanyaji wa takwimu /SENSA ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10 katika nchi yetu. Na hii ya mwaka huu ni SENSA ya sita kufanyika.
Baada ya uhuru na muungano nchi yetu imeendesha zoezi hili la SENSA mala tano kwa mtiririko huu, 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012 na hii ya mwaka huu 2022 inafanyika kwa mara ya sita.
Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 imeonesha aina ya makosa yanayoweza kutendeka katika utekelezaji wa shughuli za ukusanyaji wa takwimu rasmi na adhabu zinazoweza kutolewa dhidi ya mtu aliyethibitika kutenda makosa hayo.
1. Ni kosa kisheria kwa mtu yoyote kutumia taarifa za kitakwimu kwa manufaa yake binafsi. Mtu yoyote ambaye, kwa mujibu wa nafasi yake anapata taarifa yoyote inayoweza kuathiri thamani ya soko la hisa yoyote au amana zingine, riba, bidhaa au kitu na ambaye kabla ya taarifa hizo hazijatolewa rasmi kwa umma anaitumia moja kwa moja taarifa hizo au kwa kificho kwa manufaa binafsi atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu. (Breach of privacy and use of information for personal gain)
2. Ni kosa kisheria kutoa taarifa za kitakwimu rasmi bila kibali. Mtu yoyote ambaye bila mamlaka halali, anachapisha au kutoa kwa mtu mwingine taarifa ambayo ameipata kwa mujibu wa nafasi yake atakuwa ametenda kosa. (No person shall publish any information without authority)
3. Ni kosa kisheria kutoroka au kutelekeza kazi uliyopangiwa kufanya. Ukipangiwa kufanya kazi, tafadhali unalazimika kuifanya kazi hiyo ipasavyo, ili usiwe kama NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE, mwisho wa siku ukaharibu kazi. Hapo sheria haitakuacha. Hairuhusiwi kuacha kufanya jukumu lako na kufanya mambo mengine yasiyo ya msingi.
4. Ni kosa kisheria kudai taarifa tofauti na zilizoruhusiwa kukuanywa. Hivyo, katika utekelezaji wa majukumu yake, afisa yoyote aliyepewa mamlaka ya kukusanya takwimu, haruhusiwi kudai kupewa taarifa ambazo hajaidhinishwa kuzipata.
Kuna taarifa nyingine ni siri ya mtu husika na familia yake, hivyo hatakiwi kuzitoa kwani hazitakuwa na msaada wowote katika upangaji wa maendeleo ya taifa.
Mfano: unaenda nyumbani kwa mtu na kudai akupe namba za account yake ya bank pamoja na nywira au password zake, huo ni wizi.
Au unamkuta mwanamke na kumuuliza kama mumewe anamridhisha ndani ya ndoa sio sawa. Ni swali lisilo na maana. (So, obtaining information not authorized to obtain is an offense)
5. Ni kosa kisheria kuomba, kudai au kupokea au kuchukua malipo ya aina yoyote au zawadi kutoka kwa mtu yoyote mbali na Afisa wa umma aliyeidhinishwa. Hivyo, kudai na kuchukua zawadi ya fedha, maindi, kuku au kitu chochote ni kosa kisheria. Maafisa, mtakaoaminiwana kupewa nafasi ya kukusanya takwimu, muwe makini sana ili msije mkaingia matatizoni.
Mtu yeyote, iwapo atatiwa hatiani na kuthibitika kutenda makosa haya yaliyoainishwa hapo juu atawajibika kisheria kwa kulipa faini isiyopungua milioni mbili au kutumikia kifungo kisichopungua miezi sita au vyote kwa pamoja, yaani faini na kifungo. Hii ni kwa mujibu wa kifungu Cha 43(1) Cha Sheria ya Takwimu,
The Statistics Act, [CAP: 351, R.E: 2019].
Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓
Ndugu yangu, usichoke kusoma makala hii ndefu ili izidi kujifunza mambo muhimu na ya msingi sana kwa kila mmoja wetu kuweza kutambua tukiwa tunaelekea katika zoezi zima la sensa katika nchi yetu ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania.
Unatakiwa kujua kuwa ni kosa kisheria kutoa taarifa isivyo halali. Ni kosa kwa mtu yoyote kukutwa na taarifa au kutoa taarifa za kitakwimu zilizopatikana kwa kukiuka vifungu vya Sheria ya Takwimu.
Adhabu ni kifungo kisichopungua miezi 12 au faini isiyopungua milioni tano au vyote kwa pamoja.
Hii ni kwa mujibu wa kifungu Cha 43 (2) Cha Sheria ya Takwimu,
The Statistics Act, [Cap. 351, R.E. 2019]
WhatsApp: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓 No. II
Hivyo, hutakiwi kutoa taarifa yoyote iliyopatikana kwa kukiuka vifungu vya sheria hii. Mfano, hukuruhusiwa kukusanya taarifa hizo lakini umekiuka taratibu na umezikusanya kisha kuzitoa. Endapo utakamatwa na kuthibitika kuwa umetenda kosa hilo adhabu yake ni kali sana, hivyo unapaswa kuwa makini sana.
Sasa tugeukie kwa upande wa wananchi wa kawaida. Tutazame ni makosa gani yanayoweza kutendeka na wananchi wa kawaida au respondents pindi wanapotakiwa kutoa taarifa za kitakwimu.
Wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa maafisa wa ofisi ya Takwimu au watu walioidhinishwa kukusanya taarifa za kitakwimu wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu kwa mujibu wa Sheria.
1. Ni kosa kisheria kumzuia msimamizi/ mdadisi/ au karani wa sensa (authorized officer) kutekeleza majukumu yake.
2. Ni kosa kisheria kukataa au kuacha kwa makusudi kujaza fomu au nyaraka yoyote iliyokabidhiwa kwa mhojiwa(mwananchi) kwa lengo maalum. Unatakiwa ujibu maswali unayoulizwa ili kufanikisha zoezi hilo la ukusanyaji wa takwimu nchini.
3. Hutakiwi kutoa taarifa za uongo au taarifa ambazo sio sahihi, iwe kwa maandishi au kwa majibu ya mdomo. Hupaswi kudanganya kwa makusudi kwani kwa kufanya hivyo utapelekea upatikanaji wa taarifa ambazo sio za kweli na hazitakuwa na faida kwa maendeleo ya taifa.
4. Kuharibu fomu au nyaraka yoyote ni kosa kisheria. Hivyo, bila mamlaka halali hupaswi kuharibu, kuchafua au kuchana fomu au nyaraka yoyote iliyo na taarifa zilizokusanywa chini ya Sheria ya Takwimu.
5. Ni kosa kisheria kujifanya msimamizi/ mdadisi/ karani wa sensa kwa lengo la kukupatia taarifa ambazo hustahili kuzipata. Hivyo, ukijipa sifa au kujitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa ofisi ya taifa ya Takwimu hali ya kuwa sio kweli, sheria haitakuacha salama.
6. Ni kosa kisheria kumshawishi, kumhamasisha au kimshauri mtu mwingine yeyote hasishiriki katika zoezi la kitakwimu linaloendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu.
7. Hairuhusiwi kukataa kutoa nyaraka zozote zinazohusika katika shughuli za kitakwimu au kufanya kitendo chochote ambacho hakiruhusiwi kufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu.
Ukiukwaji wa masharti haya yaliyoainishwa hapo juu ni kosa kisheria na iwapo atatiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua milioni tano au kutumikia kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili (12) au vyote kwa pamoja yaani faini na kifungo.
Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 43(3) (a-i) cha Sheria ya Takwimu,

Ahsante kwa kusoma kwa makini, sina shaka kuwa umejifunza na upo tayari kutii sheria.
"Sensa ya maendeleo ya watu na makazi #Jiandaekuhesabiwa2022"
Ahsante.
It's me a Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis. 0713736006