Makosa ya kimsamiati tunayoyafanya katika kutamka au kuandika Kiswahili

Makosa ya kimsamiati tunayoyafanya katika kutamka au kuandika Kiswahili

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam ndugu zangu,

Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazokua kwa kasi kwa sasa ulimwenguni. Lugha hii inazidi kusambaa Kijiografia pamoja na kuongeza idadi ya wazungumzaji kila kukicha.

Pamoja na mafanikio haya ya lugha ya Kiswahili bado watumiaji wake wengi wanafanya makosa mbalimbali katika matumizi ya misamiati, sentensi, mantiki, matamshi na uandishi.

Tuutumie uzi huu kufahamishana makosa ya lugha yaliyozoeleka pamoja na usahihi wake.

1. Misamiati

Makosa
Usahihi
KurogaKuloga
HovyoOvyo
UwongoUongo
NilikuaNilikuwa
UmaskiniUmasikini
HatimaHatma
FikiraFikra
AiiuwawaAliuawa
NdioNdiyo
MaswalaMasuala
SioSiyo

Je, maneno gani mengine unayoyafahamu?

Karibu uchangie tujifunze
 
Shukrani nimepata kitu.

Hapo juu "shukrani" nipo sahihi?
 
Back
Top Bottom