Makosa ya kiprotokali katika 'barua ya Nchimbi'

Ukiisoma kwa umakini ni kama anaijulisha ofisi ya makamu wa rais kuwa amesha muandikia rais barua ya kujiuzulu, maana yake kuna barua ya kwanza imeenda ofisi ya rais.

Swali la kujiuliza barua ya kujiuzulu ameikabidhi lini? Atakuwa ameona wanachelewesha kumjibu kaamua kuitaarifu ofisi anayo itumikia ?
Kwamba rais akiendelea kukaa kimya na barua bado atajiondoa ofisini tarehe aliyo itaja?
Tutajua mbeleni
 
Kuna tofauti kubwa hasa pale unaona bosi wako haeleweki na zaidi anasikiliza machawa zaidi, Kumbuka hata JK hakutaka Lowasa ajiuzulu Lowasa alijiuzulu kwasababu ya uwaziri mkuu ambao samweli sita ndiye aliyekuwa aupate hivyo kwasababu ya hasira za Lowasa na kule kujiamini aliamua kujiuzulu.
 
Bora kosa kulioko angeandika halafu akashinikizwa kubali uwamuzi wake.
 
Umeambiwa kosa hilo pia alilifanya waziri mkuu lowasa
 

Hata Lowasa, Ndugai na Mpango hawakujiuzulu kwa kufuata protocol. Ndiyo CCM hiyo ya sasa. Polepole alisema ni Wahuni wanaongoza nchi. Wameipiga serikali photo copy.
 
Yuko sahihi ata polepole aliandika taarifa kwa umma...
 
Waacheni waauaji wauane!
Kwani nini?
 
Wh ar Yu📍
Wakati mwingine unaweza kuandika barua usijibiwe Kwa wakati hivyo unaweza kujikuta umenyanganywa kiti ata kama ulikuwa unampango wa kutoka unajikuta upo NJE. Ndo alichofanya polepole. Siasa za Tanzania zimejaa timing ndo maana viongozi wengine wanakosa protocali.
Tuiombee nchi yetu. Tupate katiba mpya
 
Point of no return, one way tiket.
Hoja yako haina faida kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…