Makosa ya kiprotokali katika 'barua ya Nchimbi'

Protokali wakati ya no longer?
 
Clearly msg sent and delivered

BTW hakuna kosa lolote la kiprotokali hapo

Makamu kuandika barua ni HAKI yake na halazimiki na protokali yoyote kutangaza kafanya hivyo…….. sana sana kasaidia kuondoa SINTOFAHAMU ambayo ingejitokeza iwapo Rais angetangaza na kuteua mwingine kwasababu kwa siasa za ccm zilipofikia watu wangeleta hadithi kama za Ndugai

Hata hivyo watu bado wanajiuliza isije ikawa yuko chini ya ULINZI na wasiojulikana wakafanya yao kwenye acc yake ya Insta kutangaza kajiuzulu 😂
 
Tofautisha taarifa kwa umma na barua ya kujiuzulu. Wewe protokali unaijua vema kuliko wao
 
Nyie wajuba bana.. yaani barua ya nchimbi aitangaze rais. Kwa nini uone mwenyewe kufanya sio sawa. Maana ake hahitaji kukataliwa.

Kama hukubaliani jambo huhitaji kufanya majadiliano.

Ukiwaachia wanaweza kukubagaza na barua yako wanayo.
 
Kuna wakt inabidi uandikiwe haraka haraka mambo yaendeee
 
Kikubwa ameshajiuzulu na mhusika ameridhia hayo ya protokali kaa nayo mwenyewe, inaonekana huko juu kwa moto hata mwaka hajamaliza?
 
 
Sio kweli, Kikwete ni mnafiki mkubwa wewe humjui tu, yeye ndiye aliyemchora Lowassa halafu akampa Sitta Assist akamalizia Goli.

Kikwete alitaka aje aweke pandikizi lake kwenye kiti cha urais ili baadaye ndoto yake ya mtoto wake kuja kuwa rais ije itimie siku moja na alijua fika kwamba endapo Lowassa angeukwaa urais hiyo ndoto yake ingeyeyuka.

Baada ya hapo ndipo akawekeza kwa Samia sasa na kuweza kufufua ndoto yake hiyo tena.

Wewe hujui mambo bwana, lakini hata hivyo ndoto hii itazimika vibaya kabisa kwani ccm hawataweza kutawala tena nchi hii beyond 2030, note this.
 
Mkuu Aleni, Allen Kilewella
Kwanza naunga mkono hoja,
Ukiteuliwa ni unateuliwa kwa barua, hivyo ukijiuluunaandika kwa mamlaka yako ya uteuzi kuomba ruhusa ya kujiuzulu.
Barua ya kukuruhusu ikiisha kujibiwa kuwa ombi lako la kujiuzulu limekubaliwa, ndipo sasa mamlaka yako ya uteuzi itatoa taarifa kwa umma kuwa Mhe rais amepokea barua ya ombi la kujiuzulu, ameridhia, na baada ya hapo ndio wewe unaweza kutoa taarifa yako kwa umma.

Kilichotokea ni VP aliwekwa Kiti Moto na kikao cha NEC akalazinishwa kujiuzulu, akagoma.

Akaandikiwa barua ya mashitaka kuhudhuria mashitaka kuhudhuria kamati ya maadili, akagoma, akijua analindwa na katiba ya JMT, rais na VP wana kinga ya kikatiba ya kutokushitakiwa na mamlaka yoyote ndani ya JMT.

Kikao cha maadili kikatoa mapendekezo yake in absentia, kuamua kumfuta uanachama, kikakabidhi kwa Secretariat, hoja ikaingizwa kwenye CC, ikapita, ikatishwa NEC kubariki

Kabla NEC haijakaa kumfukuza, yeye akatangulia kumwandikia barua mamlaka yake ya uteuzi kuomba ruhusa ya kujiuzulu.

Mamlaka yake ya uteuzi ikala kobiz ili isubiri kumtimua, ndipo yeye alipoona kimya na NEC imeitishwa, akaamua yeye kutoa taarifa kwa umma kuwa umemuandikia rais barua ya kujiuzulu. Kitendo hiki ni kinyume na protocol, ila kimesaidia, Ikulu ikatoa taarifa ya rais kukubali ombi lake la kujiuzulu.

Hata hivyo licha ya kujiuzulu mwenyewe bado NEC ya CCM wakamfukuza kwa kujifurahisha, CCM ina mamlaka ya kumfuta uanachama mwanachama wake yeyote lakini haina mamlaka ya kumuondoa VP wa JMT, hivyo licha ya kufutiwa uanachama wa CCM, Dr Nchimbi ni makamu rais mstaafu ana haki zake zote za mafao ya kustaafu na haki pia ya the right to privacy ikiwemo kuamua kutulia na kujinyamazia kimya. https://www.jamiiforums.com/threads...-iwe-rais-amepokea-taarifa-ameridhia.2466606/

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…