Makosa ya kiswahili yanayofanywa na vyombo vya habari vya Tanzania

Makosa ya kiswahili yanayofanywa na vyombo vya habari vya Tanzania

Shomari kawambwa

New Member
Joined
Mar 1, 2018
Posts
2
Reaction score
2
Inasemekana kwamba, vyombo vya habari vya Tanzania vinafanya makosa ya matamshi, maandishi na maana katika maneno, istilahi na sentensi za kiswahili sanufi.

Kutokana uvumi huo, makala hii imeona ni vyema makosa hayo yakatafitiwa na Kubainishwa usahihi wake.

Makala hii inakusudia kuchunguza na kuyabainisha makosa hayo kwa makini pamoja na kuchunguza sababu na udhaifu wa vyombo vya habari vya Tanzania katika kuyafanya makosa hayo.

Je, nimakosa yapi hayo na usahihi wake na nini kifanyike?
 
MAKOSA KATIKA UANDISHI KWENYE MAGAZETI YA KISWAHILI

Yako maneno yanayotumika katika wingi na umoja. Kwa mfano, matumizi ya neno dhumuni yamekosewa, hivyo siyo sahihi katika umoja. Neno sahihi ni madhumuni.

Napenda kuendelea na makala zangu kuhusu makosa yanayojitokeza katika uandishi kwenye magazeti ya Kiswahili hapa nchini. Mifano ni kama ifuatayo:

“Tanzania imo katika utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) wenye dhamira ya kubadili mifumo ya siasa, uchumi na jamii pia elimu.”

Lipo neno moja muhimu ambalo limebeba maana ya sentensi hii. Neno hilo ni ‘mpango’ au mkakati. Siyo sahihi kimantiki kutekeleza matokeo, bali tunatekeleza mipango au mikakati ya Matokeo Makubwa Sasa. Kwa hiyo ni sahihi kuandika “Tanzania imo katika mpango wa utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa.”

“Sauti ya Dhiki kilichovuma sana na mtunzi alifahamika aghalabu.”

Matumizi ya neno aghalabu yamekosewa. Neno aghalabu lina maana ya mara kwa mara au kwa kawaida. ENDELEA HAPA >>>>>
 
Neno "kupelekea" ni moja ya maneno ya hovyo kabisa. Mf. Uchunguzi umepelekea mtu mmoja kufukuzwa kazi. -------- badala ya umesababisha.
 
Back
Top Bottom