Mkuu, tuhepuke nadhani inatakiwa iandikwe tuepuke!Inabidi tusaidiane wana JF kuhusu hili tatizo la matamshi na uandishi wa baadhi ya maneno ya kiswahili ili tuhepuke kuharibu lugha hii,...
Yako makosa mengi yanayo jirudia ningependa nawe pia uyaainishe hapa.
hakunaga kipala kibaya kama cha Rejao badala ya hakuna kipara kibaya kama cha Rejao!Hakunaga!!
Inabidi tusaidiane wana JF kuhusu hili tatizo la matamshi na uandishi wa baadhi ya maneno ya kiswahili ili tuhepuke kuharibu lugha hii,kwa mfano;
...kura chakula,badala ya kula chakula.
...abari zako,badala ya habari zako.
...piga kula,badala ya piga kura.
...kalibu,badala ya karibu.
...hasubui,badala ya asubuhi.
...askali,badala ya askari
...malanyingi,badala ya maranyingi.
...eshima,badala ya heshima.
Yako makosa mengi yanayo jirudia ningependa nawe pia uyaainishe hapa.
Eti jamani kipi sahihi,Kusema 'analinga' au 'anaringa' ?
hiyo number 2a hayo ni maneno mawili tofauti yenye maana tofauti, huenda mtumiaji alimaanisha mazingara ktk hali ya ushirikina.Nilitaka kuanzisha thread kulalamikia usahihi wa waandishi wetu katika matumizi ya lugha ya kiswahili, lakini acha niongezee haphapa kwako mkuu,
1. Masuala mazima..... badala ya suala zima
2. Mazingara badala ya mazingira
2. Lisaa badala ya saa, masaa badala ya saa.
asante mkuu