Makosa ya Mwalimu na Msimamizi yametuponza wanafunzi

yassin12

Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
10
Reaction score
0
mimi kwa jina naitwa Yassin Said Athumani ni
kijana ninaeishi morogoro ni mmoja kati ya
wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne
katika shule ya Jabal hiraa seminary school lakini
matokeo yang yalifutwa na BARAZA LA MITIHANI
TANZANIA kwa madai kuwa katika majibu yangu
somo moja la mwisho ambalo ni computer studies
2 (plactical) kua mimi na wenzangu wanne
tumetumia takwimu sio sahihi... hvyo basi ni
uzembe ambao ulifanywa na wasimamizi pamoja
na mwanafunzi mmoja na mwalim wetu wa somo
pale shuleni... mwalim huyo wakishirikiana na
mwanafunzi walipewa fursa ya kuchukua flash disk
na kukusanya majibu yetu yote ambao sio
utaratibu na sheria za mitihani basi walitumia
nafasi hiyo kuhamisha majibu yangu na kuweka
kwa wale wengine kwa sababu walijua uwezo
wangu ktk hilo somo hapo shuleni na kuwafanya
BARAZA KUFUTA MATOKEO YANGU NA YAO PIA...
nilipeleka malalamiko hayo pale baraza la mitihani
na baada ya siku kadhaa mbele TUME ilioundwa
na WAZIRI MKUU ilikuja pale shuleni na kutuhoji
juu ya yale yaliotokea pale shuleni lakini baada ya
matokeo yoote kufutwa na kuyapanga upya basi na
mimi nilipata matumaini kuwa huenda na yangu
yakatoka ila sikuyaona roho inaniuma nina majonzi
sina wa kunisomesha tena kwa shida niliopata
kusoma kidato cha kwanza mpaka cha nne kwa
shida na tabu kubwa
NINAOMBA MSAADA WAKO WA KISHERIA AU
KAWAIDA TU NIFANYE NINI ILI BARAZA LA
MITIHANI WAWEZE KUNIPA MATOKEO YANGU NA
KUWAPA ADHABU WALE WOOTE WALIOHUSIKA JUU
YA HILI
YASSIN SAID ATHUMANI
0719715947
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…