Jinai maana yake ni makosa yanayofanywa dhidi ya umma. Kila mwananchi/raia ni sehemu ya umma, kwa kuzingatia ile dhana ya Mkataba wa Kijamii [Social Contract Theory] ya Montesquieu. Kila raia ana wajibu wa kulinda mkataba huu, lakini viongozi wanasimamia tu utekelezaji wa yote yatakayokubaliwa na raia wote kwa manufaa ya wote. Rushwa ni jinai. Ni wazi kuwa kila raia anapaswa kuzuia makosa ya jinai, ikiwa ni pamoja na kukamata (siyo kuadhibu) watenda jinai, pale inapoonekana kuwa askari polisi hayupo/hatofika kwa muda muafaka katika eneo la tukio.
Lakini ni vyema zaidi ukitoa taarifa kwa TAKUKURU, wao watakamata na kufungua mashtaka dhidi ya mtoaji/ mpokeaji wa rushwa.