Ndugu
Bakari China nikupe faida ya maneno hapo kidogo.
neno "WAMEKUWA" linatumika kuonesha viumbe hai kutoka hali fulani na kuwa katika hali fulani
hiyo herufi ya kwanza ambayo ni "W" inajulisha uwingi wa hao unaowazungumzia,yaani wakiwa kuanzia wawili ndo unatumia "WA"
Mfano : watu wamekuwa weusi.
Mbwa amekuwa mwembamba sana
Alafu neno hilo hilo ukiondoa "W" Itabaki AMEKUWA hii pia inatumika kwa kiumbe hai chochote lakini kiwe kimoja visiwe viumbe hai vingi
Mfano .
Bakari China amekuwa mjuzi Wa kiswahili
Mbuzi amekuwa mnene.
Sasa sentensi "WAMEKUWA KUTUONA" neno wamekuwa hapo halioneshi kubadilika kwa hali ya watu kutoka katika hali moka kwenda nyingine.hivyo limekaa pahala sio pake.
Hapo usahihi ni kusema "WAMEKUJA KUTUONA"
Kama kuna swali Ndugu bakari unaweza uliza bila shida.