Makosa yanayofanywa na wanaotoa elimu ya ujasiriamali

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
Kuna kitu ambacho wananchi wanakuwa wanapotea bila kujua kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaohamasisha na kutoa elimu kuhusu ujasiriamali, Sio wote


Watu hao wanawasaidia watu,lakini wanaruka sehemu kubwa ambayo inawaumiza sana
Watu wanaoamua kutumia elimu yao kwa manufaa yao,mfano kuna wale wanaotoa elimu kuhusu
Kutengeneza vitu kama sabuni,shampoo na vinginevyo,hao hutoa tangazo la kuwafundisha watu mbinu
Za kuwa mjasiriamali, wao hufundisha namna ya kutengeneza hadi unaelewa halafu wanakuacha.hilo
Ni kosa kubwa sana kwa wao kumfundisha mtu kutengeneza kitu kinachofanywa na makampuni makubwa kama kazi yao halafu ukamfundisha yeye kwa shilingi elfu 30, bila kujua atatoka hapo atatafuta fedha ya mtaji na mtaji wa kwanza unaweza kuwa ni 50,000 tu hapo ameshapigia hesabu akiuza anauhakika wa kutengeneza fedha nyingi halafu inakuwa tofauti.

kwa muendelezo zaidi bonyeza hapa chini


Elisha Chuma: Makosa yanayofanywa na wanaotoa elimu ya ujasiriamali
 
Mkuu hatuna muda wa kufungua huko, wewe post kitu chote,

Kwanza hakuna Elimu ya Ujasiriamali kuna elimu ya Biashara, Na hao unao ongelea wanafanya biashara kama unavyo fanya wewe hapa mkuu kwa nini tufichane?

Hiki kinacho itwa elimu ya kuwa mjasiriamali ni biashara na ilianzia Ulaya na kwa sasa iko kila mahali, na inafanywa na kila mtu,

MTU KUWA MJASIRIAMALI HAHITAJI ELIMU YA AINA YOYOTE ILE ILA MJASIRIMALI KU EXPAND ANAHITAJI ELIMU YA KIBIASHARA, Hakunaga elimu ya Kijasiriamali
 
Mkuu, nilishaandika pia tofauti za elimu hizo na tofauti kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara hivyo sasa hivi ninafanya muendelezo wa kile nilichokianzisha.

Ila kuna tofauti elimu ya ujasiriamali ni elimu unayopewa kwa ajili ya kukutengenezea njia za kujiajiri na kujiongezea kipato na elimu ya kibiashara ni elimu unayopewa kwa ajili ya kuendesha na kuimiliki vizuri biashara yako

Hivyo elimu zote zipo mtu anaekuja kukufundisha kutengeneza sabuni na shampoo huyo anakufundisha ujasiriamali na mtu anaekuja kukufundisha namna ya kuendesha na kukimiliki ulichojifunza hapo anakufundisha biashara kuna tofauti mkuu

Jaribu kupitia machapisho yangu ya nyuma nadhani utanielewa zaidi

Asante
 

I beg to differ mkuu, mtu anekuja kukufundisha kutengeneza sabuni si kwamba anakufundisha ujasiriamali, ni kama aliekufundisha kuendesha gari, kulima, kucheza soka etc..... Ujasiriamali kama ujasiriamali ni kitu ambacho si rahisi kufundishika kama wengi wanavyodhani au wengi manvyotaka kuaminisha watu. Ujasiriamali Ni ujuzi/akili/uwezo wa kugeuza mazingira na maarifa/taarifa ulizo nazo kuwa pesa au kuwa mafanikio. Mfano mzuri ni kwamba wengi wa hao hao waalimu wanaojiita ni waujasiriamali wengi si wajasiriamali. bali ni watu wenye ujuzi wa kutengeneza sabuni.
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu hayo mafunzo ya ujasiriamali wanayoyatangaza.

Nimefurahi kuona wengi mmeshtukia. Nilikua najiuliza eti mafunzo ya kutengeneza sabuni, mafunzo ya kuchanganya rangi za kupaka gari (hauna hata garage nani ataleta gari lake ulisiribe hiyo mirangi yako?)

Nionavyo mie elimu au mafunzo yanayowasaidia wajasiriamali ni jinsi ya kuthaminisha kile wanachokibuni katika kuwaongezea kipato kama vile elimu ya biashara (kutunza kumbukumbu na umuhimu wake, kupanga mapato na matumizi, elimu ya mikopo, utunzaji akiba na uwekezaji mdogomdogo)

Elimu hiyo niliyotaja ni pana sana na inachukua miaka kuihitimu hivyo basi hawa wajasiriamali inatakiwa tushare nao kwa uchache vitu vya msingi ili viwasaidie maana hawana uwezo mkubwa wa kifedha kujisomesha lakini pia hata muda mwingi kwaajili ya kusoma hivyo unawapa vitu vichache vya msingi ambavyo wanaweza kwenda kuvifanya ktk maeneo yao na kazi za kila siku.
 


Jaribu kufuatilia kwa makini wanaotangaza kutoa semina za ujasiriamali utakubaliana na mimi mkuu

Tena kwa ada ya 10,000 hadi 25,000
 
Usimfunge Ng'ombe kinywa apurapo nafaka.
 
Elimu ni nyenzo inayomuwezesha mtu kufikia lengo lake kwa urahisi na ufanisi ingawa bila elimu anaweza pia kwa kukosea na kurudia hadi afanikiwe. Elimu ni vizuri itolewe kwa wale ambao tayari wameishazitambua fursa, wameishaanza na wanahitaji ufanisi zaidi ktk biashara zao. Tatizo ni kuwa watoa elimu hawawajulishi hivyo matokeo yake kundi zima linaenda kuanza kutengeneza sabuni, lishe, batick na kwa vile ni wa eneo moja supply inaongezeka kuliko demand na hawana uelewa wala uwezo wa kutafuta soko nje ya eneo lao....mtaji unakufa na vile hawakuwa na hata spirit ya kulisimamia hilo wazo ndio wengi wanakata tamaa na vitabu na mafunzo yanakuwa hayana maana kwao. Ukweli ni kuwa mjasiriamali anachotakiwa ni kujitolea au kuwa under mentorship ya mkongwe ambaye unataka kuifuata biashara yake. Humo utajifunza jinsi ya kufanya ufanikiwe. Ni bora waelimishaji wawaeleze kuwa uwe umeisha au unafanya biashara unayotaka kufundishwa. Wawafundishe toka mwanzo fursa, lengo na mitaji na mapato kama wanavyofanya wenye business plan ili kidogo wafunguke macho wasiingie kichwakichwa. Ni mtazamo wangu.
 
asante @ mama Joe

ni kweli wanapotosha sana na inatakiwa watanzania kuamka mapema kuligundua hilo wale walimu wako kipesa zaidi na sio kikusaidia watu, japo sijui kama hata wao wanauelewa wa kutosha na vitu wanavyofundisha na kuvifanyia kazi
 
Hawa watu mm naona bora wapongzwe make binafsi nimewah kuudhuria semina ya Dr.Didas Lunyungu imenisaidia sana.Ningesema namilik nn ila najua watasema najiproud.Unajua hapa Tz kadri unavyosoma sana ndo unazid kufanya maisha yawe magumu.Make tunajifanya kujua mno wakat kaz hatuna kuponda kwiiiiing.Wakat hata mia huna ila unajisifu mm msomi.Binafsi kuna watu leo wanaponda watu hw humu wakat waki ''log out'' unasikia wanaomba cc 2liopata mafunzo mara oooooh nna nembo nzuri nchagie, nipe dili la vifungashio.Hv nnapokupa hilo dili hujui bila watu hawa usingekula? mbna humuomb Mengi au Bakhresa tenda ya vifungashio? c ndo huwa mnawasifia.Najua huwez kwenda kwakuwa hata ww msing mdogo unahitaji hwa waliofundshwa na walimu hawa kwan ndo 'size' yako..AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.
 

Yanaweza yakawa ya kweli unayosema mkuu ila mwanzo kabisa wa uzi huu umeandika sio wote lakini pia nachelelea kukubaliana na wewe sababu kama umekuja kumuelimisha mjasiriamali mdogo hayo yote inaweza kumsaidia lakini hebu angalia gharama zake kama ni za mjasiriamali mdogo kuanzia kutengeneza bidhaa yote kuandaa sehemu ya kuweka kutengeneza logo na kufungasha kweli ni ya mtu wa hali ya chini na bado unamuandaa apambane na washindani ambao wanafanya hiyo biashara toka zamani, kwa haraka haraka ni hapana sababu gharama ni kubwa kuliko faida yake, mfano hai leo hii ukitaka kutengeneza kadi za harusi unaweza kulipia hadi Tshs.3000 kwa kadi moja ya kawaida tu lakini unaweza kwenda kununua zilizotengenezwa kabisa ( ready made) ukakuta bei yake ni 700 au 1000 tshs.kwann? sababu wanatengeneza nyingi sana ambapo gharama za uzalishaji na kila kitu kinaweza unganishwa kwa hiyo 700 na bado wakapata faida.
 
Elisha Chuma
mkuu hata mm nakubali mtaji ni changamoto ila pesa bila kujua ni kipi ufanye hilo ni tatizo kubwa ndo maana unaona 'post' nyng mara nna m.3 nifanye nn.Mfno kwnye semina za Lunyugu anakupa mbnu za soko,customer care,vpeperush vyenye bei za ''rawmaterials'' kwahyo kabla ya kutengneza unajua cost zake faida yake n.k.Tatizo kubwa lipo kwa cc wajasiliamali,mfno bdhaa nyingi zipo Dsm kuliko mikoan.Watu hawa wanafundsha nenden mikoan wa2 hawaendi ingawa hata hii ina sababu yake.Naomba niisemee kwan wengi watasema ni pesa sio kweli tatzo weng wa wahtimu ni wamama unakuta kuruhusiwa na waume zao ili kwenda kutafta taarifa za,soko ni shida kweli.Mm huwa natoa muda wa kwenda mikoan na hata mipakan ili kuwanasa wateja wa nje.Hata sasa nipo mikoan natafta soko na nshapata oda Burundi ndo bado naishughrikia.Kwa hyo walimu mm nnaowajua wako sawa tatzo ni ww unayachukulia vp mafunzo yao na mfno Dr.Lunyungu kawapa kundi fulan la wamama m.2 baada ya wao kupambana wakapata soko Kenya.
 
Last edited by a moderator:


"anakufundisha ujasiriamali, ni kama aliekufundisha kuendesha gari, kulima, kucheza soka etc..... Ujasiriamali kama ujasiriamali ni kitu ambacho si rahisi kufundishika kama wengi wanavyodhani au wengi manvyotaka kuaminisha watu. Ujasiriamali Ni ujuzi/akili/uwezo wa kugeuza mazingira na maarifa/taarifa ulizo nazo kuwa pesa au kuwa mafanikio. Mfano mzuri ni kwamba wengi wa hao hao waalimu wanaojiita ni waujasiriamali wengi si wajasiriamali. bali ni watu wenye ujuzi wa kutengeneza sabuni"nukuu
 
du hivi hadi leo kuna watu hawajui umuhimu wa elimu kwel wa tz kaz tunayo hiv mwaka wa 2013 ndo uanze kukaa chini kumfundisha mtu umuhimu wa elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…