Grateful for so much
New Member
- Jun 4, 2023
- 1
- 2
Ni saa 1 usiku, nakatiza maeneo ya Kimara, Dar es Salaam ili nikaunganishe usafiri wa kwenda nyumbani baada ya pilikapilika za kila siku.
Mara naona kijana akikatiza mbele yangu kando ya viunga vya Kimara mwisho akiwa ameziba sura yake kwa maski.
Namkodolea kijana huyu aliyevaa koti kubwa jeusi kwa dakika 3 hadi 5 huku nijiuliza maski ile itakuwa ni ya kazi gani, maana haifanani na zile za Uvuko-19 badala yake ni zile ambazo tumekuwa tukiziona katika filamu kwa watu wanaofanya uhalifu.
“... unashangaa…? Hapo mwenzako yuko kazini…” ilikuwa ni sauti iliyonishtua kutoka kwa mtu niliyekuwa nimeongozana naye kwenye uelekeo wangu.
Kama ilivyo jadi yetu Watanzania, nalazimika kumsalimia mwenzangu huyu ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Mwando Juma (si jina lake halisi).
Kwa shahuku ya kutaka kujua zaidi nalazimika kuongozana naye bila kujali kuchelewa kufika nyumbani.
“Kaka samahani tunaweza kuzungumza kwa kirefu maana nimevutiwa na hiki kisa na natamani tukae mahala unieleze,” nilimuomba Mwando.
Hata hivyo, aliniambia kwa muda ule asingeweza kunieleza kwa kina badala yake tutafute ziku nyingine kwani nawafahamu jamaa hao na hapo unavyoona wansambaza dawa za kulevya.
Nilimwelewa kwa muda huo lakini sikushawishika kupuuzia kuujua uhusiano kati ya kile nilichokiona kwa kijana aliyepita mbele yetu na nilichoambiwa baada ya kuonesha hali ya kushangaa.
Dawa za kulevya, na maski usoni muda huu? Ni moja ya jambo lililonichanganya sana na kutamani ahadi ya kukutana na Mwando itimie kama tulivyozungumza.
Siku nyingine isiyokuwa na jina ahadi yangu ya kukutana Mwando imetimia kwa ajili yakupata ufafanuzi wa kile nilichokiona.
Kwa mwonekano, Mwando ni kijana wa rika la kati, mtanashati, maji ya kunde na mcha Mungu. Hata hivyo, wakati tukiendelea kuzungumza nabaini kwamba ana uelewa na taarifa nyingi kuhusu njia za usambazaji wa dawa za kulevya.
Baada ya kumwonesha kiu ya kujua mengi, sikutegemea kama angekuwa na taarifa nyingi kiasi kile.
Mwando anadai kijana yule kwanza amevaa vile ili kuficha sura yake asijulikane kwakuwa anakuwa amebeba mzigo wa dawa za kulevya aina ya cocaine na heroine kwenye begi.
“Muda mwingine kama anakuwa hana begi basi wanavaa makoti yanayowawezesha kubeba mzigo huo. Kijana kama huyo uliyemuona anakuwa anachukua mzigo kutoka kwa mkubwa wake aliyemwagiza kwenda kwa mkubwa mwingine ambaye ni mpokeaji na kuanza mnyororo wa usambazaji mpaka kufikia mtumiaji wa mwisho ambao ndiyo hawa vijana mnaowaona wanalalama mitaani,” anasema Mwando.
Mnyororo unaanzia wapi
Baada ya kumuuliza swali hili Mwando anacheka kidogo kisha ananiambia kuwa kuna mzunguko mrefu ukihusisha raia wa kigeni.
“… unajua mnyororo wa hii biashara unaanzia kwa mmiliki huwa wanaitwa mzungu wa unga kwenda kwa middle man (mtu wa kati), ambaye naye ana vijana wake wanaopeleka kwa watu wao wanaojulikana kama sadali, kisha wao ndiyo wanauzia watumiaji,” anasema Mwando.
Sasa hawa tulio waona siku ile ni akina nani kwenye hili kundi?
Mwando anasema vijana hao ni wa mtu wa kati (Middle Man): “Hawa sasa kazi yao ni kupeleka mzigo kwa watu wanaofahamika kama sadali kisha wao ndiyo wanauzia watumiaji wa mwisho,” anasema Mwando.
Licha ya Mwando kukiri kwamba siyo sehemu ya watumiaji wa dawa hizo, lakini ameanza kufahamu mbinu mbalimbali za usambazaji ikiwamo hiyo.
Anajuaje mbinu hizi?
Kulingana na maelezo yake, anasema akiwa na umri mdogo alikulia sana maeneo ya Manzese, Dar es Salaam ambapo ndiyo moja ya eneo utakapokutana na watumiaji wa dawa hizo mpaka leo.
“Nilipokuwa mdogo ilikuwa ikifika muda fulani baba alikuwa akinikataza kutoka nje au kupita njia fulani kwasababu ya matukio kama hayo, hivyo nimekuwa nikijua mbinu hizo, ndiyo sababu sishangazwi na lolote,” anasema Mwando.
Watumiaji wanasemaje?
Baada ya kufunguliwa macho na Mwando nilijipa kazi kuhakikisha napata moja wapo ya watu wanaoguswa na cheni, kwa maana ya watumiaji wenyewe.
Nakutana na Shengo (si jina lake halisi) huyu mmoja ya watumiaji wa dawa za kulevya kwa miaka 15 sasa.
Shengo, alianza matumizi ya dawa za kulevya baada ya maisha magumu aliyopitia ya kutokuwa na malezi ya wazazi wote wawili baada ya baba yake kumkataa na mama yake kufariki dunia, hivyo akaamua kuingia mtaani kufanya shughuli alizoamini zingempa japo Sh 500 ya chai na maandazi.
“Maisha yangu hayajawahi kuwa mepesi, nimepitia maisha magumu sana. Usinione hivi nyuma nimeshakuwa mwizi, nimeingia kwenye baa kucheza muziki ili nitunzwe, nimeshakuwa mpanga viti kwenye kumbi za shughuli mbalimbali yote ili tu niweze kuishi mjini hapa,” anasimulia Shengo kwa mifano akinionesha baadhi ya picha zake za zamani katika ukurasa wake wa Facebook.
Baada ya kumwelezea Shengo kile nilichokiona kwa vijana wale, aliniambia njia hiyo siyo maarufu na ni njia inayotumika sana sana na wenyewe wakubwa ili kuleta mzigo mtaani.
“Vipi unataka nikuunganishe na Senior (mzoefu) wangu nini?,” aliniuliza Shengo baada ya kuona nazungumza naye lugha ya kuonesha nahitaji kuja kuwa mtumiaji.
Gharama yake ni kiasi gani?
Kulingana na Shengo, gharama kwa kipimo inategemea na ubora wa mzigo.
“Unajua hizi dawa zinakuwa na madaraja makuu manne, mzigo unaoletwa mtaani ni uliochakachuliwa kwenda daraja la chini grade ya chini kabisa ambayo huuzwa Sh 150,000 kwa ukucha mdogo ambao ndio hutumika kama kipimo.
“Lakini watu kama sisi hatuwezi kumudu hiyo hela, tuna ile ya kwetu inayochakachuliwa kutoka kwenye daraja la mwisho la nne ndiyo tunapata mtaani kwa 2,000 angalau wote tupate,” anasema Shengo akionekana kunishawishi kuingia na kuwa mteja.
“Sawa, bora nimejua, nitakushtua”, nilimjibu Shengo akionesha utayari wa kuniunganisha na mkubwa wake japo alitoa angalizo kuwa hatanipa mawasiliano yake au kunipeleka kwake.
Nini kifanyike?
Ukweli kuhusu matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya umekuwa ukiwaathiri watu na jamii kwa muda mrefu. Isivyobahati shughuli hii imejificha katika maeneo mengi, ikisababisha athari kubwa kwa watu wanaohusika na watumiaji wa dawa za kulevya na jamii kwa ujumla.
Ni muhimu kuwa na ufahamu zaidi na kufanya mabadiliko ili kushughulikia tatizo hili.
Serikali, mashirika ya kiraia, na jamii kwa ujumla ni muhimu kuchukua hatua za haraka kushughulikia hatari iliyofichwa ya matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya.
Karibuni, Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) pia imebaini mbinu mpya za usafirishaji wa dawa za kulevya ikiwemo raia wa kigeni kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na wanawake wa kitanzania zaidi ya mmoja na kuficha dawa za kulevya kwenye makazi ya wanawake hao huku wao wakipanga nyumba tofauti na wanakoishi wapenzi wao.

Upvote
5