Za leo jamani,
Mimi na swali hivi mtu kanyoa ndevu vizuri tuu ila sio mpaka chini, bado katokwa na vidonda kama vile vya kunyoa mpaka kwenye ngozi nadhani mnavifahamu then pakawa panatoa harufu nyingine mbaya sana kama ya uozo, hivi nini hasa tatizo na jee mtu huyu afanye nini. Kwa kweli ameshatumia baadhi na aftershave na vyinyolea mbali mbali ila wapi! Noambeni msaada wenu JF Doctors.
Hiyo mashine ndo anatumia kwa sasa angalao vipele vilipungua kidogo ila harufu sasa ndo balaa... na yeye yuko Denmark. Siunaelewa tena mambo ya huku mikumbato kwa sana tuu...imebidi nimwambie asitishe kwa mda tupate sulu kwanza. Maana ni noma utafikiri bafu haendi ilihali ni twice a day. Asante kwa ushauri wako ndugu.
Penny, mwambie atumie mashine ya kunyolea nywele jino alitoe, hii inawasaidia sana watu walio na sensitive skin. Pia kama alipata infection anywe antibiotics for 7 days straight labda itamsaidia.
Za leo jamani,
Mimi na swali hivi mtu kanyoa ndevu vizuri tuu ila sio mpaka chini, bado katokwa na vidonda kama vile vya kunyoa mpaka kwenye ngozi nadhani mnavifahamu then pakawa panatoa harufu nyingine mbaya sana kama ya uozo, hivi nini hasa tatizo na jee mtu huyu afanye nini. Kwa kweli ameshatumia baadhi na aftershave na vyinyolea mbali mbali ila wapi! Noambeni msaada wenu JF Doctors.
ushauri wangu me naona akamwone Dematologist ndio anaweza kumpa tiba sahihi.
Shem, sio my beiberry, No, no,no huyu jamaa wetu wakaribu tuu. Jamani asanteni kwa ushauri mlionipa na mbarikiwe sana.Huh!?!?!? Najua haiwezekani akawa ngosha Balantanda kwa sababu najua yeye personal hygiene na appearance anaitilia maanani sana.
Huyo mtu inabidi aende akamwone mtaalamu wa ngozi na magonjwa yake (Dermatologist). Akishapata ufumbuzi wa tatizo lake, ni muhimu awe anaenda kwa kinyozi kunyolewa hizo ndevu unless anazinyoa kila siku.
Pia, kuna vitu vingine kama wax (i.e. products like Nair for men) zinazotoa nywele kwa kumomonyoa. Au anaweza akajaribu njia ya permanent laser hair removal. Lakini kabla ya kujaribu njia hizi mbili, ni busara aende kwanza kwa huyo daktari wa ngozi na magonjwa yake angalau akapate ushauri wa kitaalamu kwanza kabla hajaamua ni njia ipi aifuate.