Maktaba Kuu ya Taifa

Maktaba Kuu ya Taifa

0890

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
28
Reaction score
42
Natumaini ndugu ni wazima katika harakati za kurijenga taifa.

Katika nchi yeyote ile elimu ni jambo muhimu sana ili kusaidia taifa kuendelea, kwa mtazamo wangu sioni kama taifa tunaweka nguvu nyingi katika kukuza elimu yetu na miundombinu yake.

Nyumba imara ni ile yenye msingi imara sio paa zuri japo paa lina umuhimu wake.

Leo nimetembelea Maktaba kuu ya taifa kujisomea, niliyoyaona nimeumia sana.

Maktaba yetu kuu ya taifa hata sehemu za kuchajia laptop zimealibika, na hili mpaka viongozi wa serikali waone ndio mambo yawe sawa kweli.

Mazingira nayo sio mazuri kwa kusoma na ndio maktaba yetu ya taifa kwelii jamani; ebu tujifunze tunapoenda nchi za watu.

Viongozi wa maktaba kuu ya taifa kama mtaona naomba muiboleshe maktaba yetu na muhamasishe watu kujisomea maana mnachokifanya hapa nikukatisha watu tamaa.

Mtu ni mwanachama wa Maktaba, unakuja na gari yako uje kusoma unatakiwa ulipie parking mhhhhh ebu tafuteni vyanzo vingine vya mapato kama pesa tunazolipa za uwanachama hazitoshi.
 
Toka 2016 wanafanya hivyo. Labda mgeni hapo.* Elimu unaifuata pale?, You must be joking*
 
Tunafahamu kuwa jengo la Maktaba Kuu ya Taifa linafanyiwa matengenezo toka mwa jana, lakini je -: Matengenezo haya yatakamilika lini ? Kwanini simu kuu haipokelewi ili wanachama waliositishiwa huduma wapewe mrejesho ? Je wanachama watafidiwaje kwa sitisho hilo ? Na lini huduma zitarejeshwa tena ? Tunaomba majibu.
 
Back
Top Bottom