Maktaba ya CCM Dodoma

Maktaba ya CCM Dodoma

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MAKTABA YA CCM DODOMA

Maktaba ya CCM Dodoma imesheheni vitabu vingi na majarida mengi.

Mara ya mwisho miaka mingi iliyopita nilipokuwa hapo maktaba ilikuwa chumba kitupu mfano wa ukumbi mrefu wenye viti na meza mtu akakaa na kujisomea.

Leo Maktaba ya CCM ni Maktaba hasa yenye meza na viti vilivyotengenezwa kwa ajili ya maktaba.
Unahitaji muda kutembelea mitaa ya maktaba hii.

Nimefarijika kukuta chini kabla ya kupanda gorofa ya kwanza ilipo maktaba kumewekwa picha nyingi za CCM na chache za TANU wakati wa kupigania uhuru.

Bahati mbaya sana katika picha hizi picha za chama cha TANU zimekosekana picha za wazalendo waasisi wa African Association 1929 na halikadhalika wazalendo waliounda TANU 1954 na wakailea na kuijenga hadi Tanganyika ilipopandisha bendera yake mwaka wa 1961.

Hapa sikusudii picha ya waasisi wa TANU wale watu 17.

Nakusudia wazalendo wengine waliomuunga mkono Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kufanya mengi ya kutukuka lakini bado michango yao haijatambuliwa.

Hapa ndipo pakutundikwa picha za wazalendo kama Ali Msham wa Magomeni Mapipa, Msham Awadhi wa Mikindani, Bi. Aza wa Kilwa, Bi. Sharifa bint Mzee wa Lindi, Bi. Mwamtoro bint Chuma wa Mtaa wa Kariakoo kwa kuwataja wachache.

Halikadhalika patundikwe ndugu zetu kutoka nchi jirani waliojiunga na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir kutoka Zanzibar, Denis Phombeah kutoka Nyasaland na Dome Okochi Budohi kutoka Kenya.

CCM wanastahili pongezi kwa kutupa maktaba hii.
Naamini kabisa inahitaji juhudi ndogo sana kuboresha sehemu hii kwa picha adimu za wazalendo hawa.

1738862457733.png

1738862542207.png

1738862577975.png

1738862667190.png
 
Shekh Said sijaona Tanzia ya Ahmed Rajab, huna lolote la kumzungumzia Ahmed?
 
Back
Top Bottom