Maktaba ya Kiswahili Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia ni hatua ya kupongezwa

Maktaba ya Kiswahili Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia ni hatua ya kupongezwa

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetoa taarifa ya kufunguliwa rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek, nchini Namibia.

Lililonivutia katika hatua hii muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasiani ni uamuzi wa ubalozi kufungua maktaba ndogo yenye vitabu na majarida ya Kiswahili kwa ajili ya watu wenye nia ya kujifunza kiswahili kuja kujisomea.

Hii ni hatua muhimu na ya kupongezwa hasa katika kipindi hiki ambacho serikali inafanya jitihada za makusudi za kuhakikisha Kiswahili kinatangazwa na kuenea kwa kasi kupitia Balozi zake, vyuo vya kimataifa na majukwaa mbalimbali ya kimataifa.

Pia Serikali za Tanzania na Namibia zipo kwenye mazungumzo ya lugha ya Kiswahili kuwa sehemu ya lugha ya chaguo katika shule za Namibia, jambo ambalo litatoa fursa za ajira kwa wataalamu wetu wa Kiswahili.
 
Back
Top Bottom