Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Katika watu ambao nimekutananao na kuwakuta wana maktaba kubwa za kushangaza, nitawataja watatu wengine nitawabakisha kwa siku nyingine In Shaa Allah.
Marehemu Sheikh Mohamed Ayoub wa Tanga siku nilipoingia ofisini kwake nilipigwa na butwaa. Sijui kama ile niite ofisi au ofisi yake imewekwa ndani ya maktaba.
Ukumbi mkubwa lakini ilikuwa ni ofisi yake sheikh nilielezwa. Vitabu kuanzia sakafuni hadi juu kukimbilia dari.
Na nimeambiwa vitabu vyote hivyo kasoma.
Siku alipofariki katika miaka ya 1900 mwishoni, Shariff Abdulkadir Juneid wa Kitumbini katika kumweleza Sheikh Mohamed Ayoub alisema kuwa yeye hajui Sheikh Mohamed Ayubu amesoma vitabu vingapi.
Napenda kueleza kitabu kimoja katika maktaba ya sheikh ambacho kaandika yeye mwenyewe. Kitabu hiki tunaweza kukiita kitabu cha kumsomesha mwanafunzi mzito wa kuelewa.
Hiki ni kitabu cha mwalimu.
Ilitokea mwanafunzi alipelekwa na baba yake kwenda kusoma Shamsiyya lakini kwa bahati mbaya alikuwa hajiwezi.
Waalimu wakajitahidi kumbadilisha madarasa wakijitahidi kumsomesha akashindikana ikawa taarifa amepelekewa Sheikh Mohamed Ayoub kuwa huyu mwanafunzi arudishwe nyumbani.
Kitu kama hiki kilikuwa hakijapata kutokea pale chuoni.
Hoja ya sheikh kwa wale walimu ilikuwa mradi mwanafunzi kaletwa kusoma lazima asaidiwe kujifunza hadi aelewe na mwishowe ahitimu mitihani.
Basi sheikh akampangia ratiba yake maalum yule mwanafunzi akawa anamsomesha yeye mwenyewe.
Huyu kijana akawa anapasi kila mtihani mwaka hadi mwaka na mwishowe akahitimu akapata shahada yake akarudi kwao.
Sheikh Mohamed Ayoub akaandika kitabu kiwasaidie walimu ambao wote ni wanafunzi wake jinsi ya kusomesha, "slow learners."
Walimu wa Shamsiyya wanasema moja ya hazina kubwa ya maktaba ya sheikh ni kitabu hiki.
Mtu wa pili ambae kanishangaza kwa vitabu alivyonavyo kwenye maktaba yake ni Abdilatif Abdallah.
Nitatoa maelezo hapa.
Mwaka wa 1992 nilikwenda nyumbani kwake London na hapo ndipo nilipopambana na mzigo huu mzito wa vitabu vilivyopangwa vyema kwenya rafu moja mbele ya kingine.
Macho yanachoka kuangalia.
Miaka mingi ikapita nikamtembelea Abdilatif nyumbani kwake Humburg mwaka wa 2011 nikakutana na msitu mwingine wa vitabu.
Nikamuuliza kama hivi vitabu ni vile ambavyo niliviona London miongo miwili iliyopita. Akaniambia kuwa hivi vya Ujerumani ni vingine.
Mtu wa mwisho ni Prof. Ahmed Muhidin. Nilifika nyumbani kwake Kikambala nje kidogo ya Mombasa mwaka jana.
Yeye mbali ya vitabu ana tapes za Nyerere kuanzia 1950s wakati anaanza siasa Dar es Salaam. Mikanda hii ili isiharibike ameihifadhi ndani ya jokofu.
Angalia vurugu la mabuku hayo pamoja na DVD za kila aina na maktaba ya picha.
Nimeingia nimesimama hadi naondoka wima nimesimama mimi ni kuchakura mabuku na yeye Profesa yuko nyuma yangu anajibu maswali yangu.
Sasa tumeshuka kutoka gorofani tuko chini naondoka.
Akanichukua kwenye kontena la futi 20 akalifungua.Vitabu juu ya vitabu, juu ya vitabu, juu ya vitabu.