Makubaliano ya Kibiashara ya Ushirika

Makubaliano ya Kibiashara ya Ushirika

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
1611223508566.png

Ushirika ni makubaliano ya watu wawili au zaidi ambao wanaweka pamoja Rasilimali pesa na watu ili kuanzisha biashara na kugawana faida.

Katika kuanzisha biashara ya ushirika ni muhimu kuwa na makubaliano ya ushirika ambayo yatakuwa katika maandishi, huku lengo likiwa ni kutatua migogoro ambayo inaweza kujitokeza baina ya washirika.

Makubaliano ya ushirika yatawekwa sahihi na washirika wote na yanatakiwa kuhusisha vitu vifuatavyo:-

a) Jina la Kampuni;

b)Asili ya biashara husika;

c)Majina na anuwani za washirika;

d)Eneo la biashara;

e)Mda wa ushirikiano ikiwa utakuwa umeamuliwa;

f)Kiasi cha mtaji kitakachochangiwa na kila mshirika;

g)Namna ya kugawana faida na hasara;

h)Mamlaka na majukumu ya washirika;

i)Mishahara na uondoaji wa washirika;

j)Uandaaji wa akaunti na ukaguzi wake;

k)Utaratibu wa kufutwa kwa Kampuni na;

l) Utaratibu wa utatuzi wa migogoro.
 
Upvote 0
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom