Labda kukusaidia. Utaratibu wa mirathi ni kwa kufungua mirathi mahakamani. Mahakama ndiyo inamteua msimamizi wa mirathi baada ya kikao cha familia kukaa na kupendekeza.
Pia mtu yeyote mwenye interest na mali za marehemu anaweza kuomba kuteuliwa na mahakama kuwa msimamizi wa mirathi.
Hivyo basi, kama kweli hiyo nyumba ni ya marehemu baba yenu, na kama aliipata ndani ya ndoa, basi lazima kwanza mali hiyo itengwe kiasi anachostahili kupata mjane na kinachobaki kinakuwa ni sehemu ya mali ya marehemu ambayo inastahili kurithiwa na warithi.
Hujachelewa, unaweza kuchukua hatua!