Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,470
Sikuwahi kufikiria hata siku moja kama yanayoandikwa hapa ni kweli, mara kadhaa nimefikiria ni watu ambao wameamua kufurahisha baraza.
Lakini yaliyonifika mimi pengine yanaweza kuonekana kichekesho zaidi kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuamini kama mke wangu anataka niwe nampiga ili aamini kuwa nampenda.
Nimeoa mwanamke wa Kikurya mwaka mmoja uliopita lakini kuna tabia ya ajabu ambayo mke wangu amekuwa nayo.
Kukosena kama binadamu kunatokea mara kwa mara lakini inapotokea yeye akakosea nikimweleza makosa yake na kumwambia kuwa nimemsamehe huwa namuona hana furaha.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza huyu mwanamke ni wa aina gani kwani unapokosa na mwenzako akasema amekusamehe kwa hakika ni jambo la kufurahia sana lakini kwake haikuwa hivyo.
Siku moja aliniudhi sana, Nilirudi nyumbani kama saa kumi na mbili hivi na kumkuta akiwa nyumbani hajaenda shule kumfuata mtoto.
Nilipomuuliza kwanini mpaka muda ule hajaenda kumfuata mtoto alinijibu kuwa alikuwa saluni akisuka.
Bila kumuuliza tena nilijikuta nikimpiga kibao cha nguvu na kuondoka zangu kwenda kumfuata mtoto shuleni.
Baadae niliporudi nilikutana na hali ambayo haikuwa ya kawaida, mke wangu alikuwa na furaha sana.
Nilimuuliza iwapo kumuacha mtoto shuleni mpaka muda ule lilikuwa jambo la kumfurahisha kiasi hicho.
Akiwa na raha za ajabu aliniambia kuwa siku hiyo kwa mara ya kwanza ameamini kuwa nampenda.
"Mume wangu sikijua kama unanipenda mpaka leo hii ndio nimeamini kuwa unanipenda, nami nakupenda sana mume wangu naomba nikikosea uwe unanipiga" alisema mama huyo