Makundi haya hayajatoa tamko lolote la kulaani na kukemea tukio la binti aliyebakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile

Makundi haya hayajatoa tamko lolote la kulaani na kukemea tukio la binti aliyebakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kwanza nitoe pongezi kwa chombo cha habari cha Wasafi media kipindi kinachoendeshwa na Zembwela, Maulid kitenge (mshambuliaji) na Gerald Hando, kwa kweli kila nikifungulia redio kwenye hiki kipindi na kutana na wazee wa minyama wakikumbusha na kulitaka jeshi la polisi lijitokeze hadharani kuwapa wananchi update nini kinacoendelea juu ya uchunguzi wa binti kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbie.

Japokua kuna muda wazeee wa minyama huwa wanapuyanga kwa hili nikiwa mwananchi mzalendo niliyeguswa na hili hakika nawapa HECKO

Nimesikitika sana kuona baadhi ya makundi kujitenga na jamii wakati hayo makundi bila ya jamii (watu) hawayawezi kusaivu kabisa ama kuendelea lakini limetokea tatizo kama hili haya makundi yameshindwa kabisa kukemea huu uozo.

(1) Taasisi za dini na viongozi mbalimbali wa madhehebu, siyo viongozi wa dini ya kiislamu au dini ya wakiristo, wamejitenga kabisa na jamii na wamesahau kabisa jamii(KONDO) ndiyo huwa wanawapelekea sadaka lakini kondoo wanabakwa na kulawitiwa wao wapo kimya tu hata kujitokeza kukemea kama vyombo vingine na taasisi zingine zilivyofanya, kwa hili viongozi wa dini wanapaswa kujitafakari sana tena pakubwa mno, wamesahau kabiisa kondoo wa bwana huwa wanatoa sadaka ili wao wale, huwa wananunua mchanga na mafuta na maji ya upako lakini kondoo wanabakwa wao wapo kimya tu.

(2) Wasanii wa bongo fleva na bongo Muvi, hawa huwa wakiumwa sehemu kubwa ya kukimbilia ni jamii (watu) wawachangie huwa wanalia mno lakini watu hao hao wakihitaji msaada wao huwa hawaonekani kabisa hata kuposti tu maandishi kadhaa kuwa wamechukizwa na kitendo cha binti kubakwa na kuingiliwa kiyume na maumbile wameshindwa kabisa.

Wasanii na Viongozi wa dini badilikeni, lakini pia niwapongeze baadhi ya wasanii na viongozi wa dini japokua ni walewale wa kila siku ambao huonekana kama wapo chama pinzani walionesha uthubutu wa kukemea jambo hili.

Na mwisho kabisa nilipongeze jeshi la polisi kwa kuwatia nguvuni wahuni (watuhumiwa) wanaodhaniwa kumbaka na kumlawiti binti na ninadhani haki itatendeka.
 
Kitima mapadri na waumini wake wamemuua Mandojo kanisani, hajatoa tamko
 
Katika Suuratu Yuusufu Aya Ya 40 allah anasema

إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٠﴾

(Hakuna hukumu ya haqi isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha kwamba msiabudu chochote isipokuwa Yeye Pekee. Hiyo ndio Dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.)
 
Wasanii wametoa tamko, ukienda hko Instagram pamechafukwaa
 
Katika Suuratu Yuusufu Aya Ya 40 allah anasema

إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٠﴾

(Hakuna hukumu ya haqi isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha kwamba msiabudu chochote isipokuwa Yeye Pekee. Hiyo ndio Dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.)
Ujinga ujinga tu.

Mkishabugia gongo no kuja kubwabwaja humu.

Kwahiyo polisi na mahakama wasifanye kazi yao bali Mungu.

Umeshikwa fahamu na dini tena kipumbavu.

Nb: Elimu ya dini bila ya kuchanganyia ni janga.
 
Back
Top Bottom