JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Muongozo huu wa Elimu kwa umma umeandikwa kufuatana na miongozo ya elimu ya afya ya Wizara ya afya Tanzania, Shirika la Afya Duniani –WHO. Muongozo huu una lengo la kuelimisha umma kwa kutoa elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa Corona. Lengo ni kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na Elimu sahihi ya ugonjwa wa Corona.
Kuanzia mwezi Disemba 2019, mamlaka Nchini China zilianza kuona kesi za aina mpya ya ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa, ugonjwa ulithibitika unatokana na maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Corona. Ugonjwa huu ulipewa jina la ugonjwa wa Corona-2019 kifupi COVID19. Kuanzia Disemba ugonjwa huu umesambaa kwa kasi na kuathiri dunia nzima, Tanzania ikiwa nchi mojawapo.
MAKUNDI AMBAYO YAKO HATARINI ZAIDI KUPATA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA CORONA
Watu wote wa rika zote wapo hatarini kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona. Hata hivyo, makundi yafuatayo yako hatarini zaidi kupata dalili mbaya za ugonjwa wa corona:
• Shinikizo la damu
• Magonjwa ya moyo
• Kansa
• Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
• Kifua kikuu
• Kisukari
• Wazee wenye umri zaidi ya miaka 65
Nina ugonjwa wa kisukari nifanyeje?
Watu wenye aina ya kwanza na ya pili ya kisukari wako katika hatari kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona. Iwapo unaugua kisukari na unaona dalili kama vile kukohoa na joto jingi mwilini pamoja na kushindwa kupumua unafaa kupima hali yako mara kwa mara.
Iwapo una dalili kama hizo unapaswa kusalia nyumbani kwa siku saba, na kuendelea kutumia dawa . Usiende hospitali. Unapokosa kuona dalili za virusi vya corona na unataka kumuona daktari unapaswa kumpigia simu ama kuwasiliana naye kwa kutumia mtandao badala ya kwenda kumuona ana kwa ana.
Mimi ni mzee je niko hatarini kuangamia?
Ushauri unaotoka kwa Wataalam wa Afya hadi kwa umma bila kutilia maanani umri - ni kujitahidi kuwa mbali na watu wengine ili kuzuia maambukizi. Hii ina maana kwamba mtu hafai kwenda katika maeneo yenye watu wengi ili kujumuika nao. Ni muhimu kwa wale wenye umri wa miaka 70 kwenda juu pamoja na watu wenye maradhi kwa kuwa wako hatarini kuambukiuzwa.
Ninaugua Pumu nifanyeje kujilinda dhidi ya COVID 19?
Mamlaka za afya katika mataifa mbalimbali yaliyoendelea ikiwemo Uingereza zimewashauri watu wenye Pumu kutumia inhaler mara kwa mara. Hii itasaidia kuzuia uwezekano wa mtu kukutwa na tatizo la kupumua linalosababishwa na virusi kama vile vya corona.
Mtu anapaswa kuhakikisha kuwa inhaler yake ipo karibu naye kila siku hata iwapo hana dalili za pumu. Iwapo Pumu imekuja na makali na umegundua kwamba umeathirika na maambukizi ya virusi vya corona wasiliana na maafisa wa afya.
Ninavuta sigara, je ninakabiliwa na hatari kubwa?
Deborah Arnott, Mkurugenzi Mkuu wa misaada ya kiafya nchini Uingereza, Ash, anashauri wale wanaovuta sana sigara wanapaswa kupunguza au kujaribu kuacha kabisa uvutaji wa sigara ili kupunguza hatari iwapo watapatwa na coronavirus.
"Wavutaji wa sigara wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya mfumo wa kupumua na wana uwezekano mkubwa mara mbili wa kupata maradhi ya mapafu- pneumonia kuliko wasiovuta sigara ,"
Inashauriwa kuwa hata kama haujihisi vema iwapo una magonjwa ya kudumu uendelee kutumia dawa ulizopewa za matibabu pale unapopatwa na coronavirus. Kama unahitaji kuchukua dawa muombe rafiki yako au mtu wa familia yako akuchukulie.
Je wanawake Wajawazito wanapaswa kuwa na wasiwasi?
Hakuna ushahidi kwamba wanawake wajawazito na wanawao wapo katika hatari ya maambukizi ya virusi vya corona lakini serikali zimewaomba kuchukua tahadhari ya afya yao. Kama watu wengine wajawazito wanapaswa kuchukua tahadhari ili kuzuia maambukizi.
Wameorodheshwa katika orodha ya watu walio katika hatari ya kupata maambukizi, kulingana na maafisa wa afya.
Maafisa wa afya ya wanawake wanatoa ushari ufuatao:
1. Iwapo wewe ni mjamzito kwa chini ya wiki 28 na hauugui ugonjwa wowote unapaswa kukaa mbali na umma lakini unaweza kuendelea kufanya kazi huku ukichukua tahadhari dhidi ya watu wenye maambukizi kwa kutumia vifaa vinavyokulinda.
2. Iwapo una ujauzito wa zaidi ya wiki 28 ama una ugonjwa kama vile figo , au ugonjwa wa mapafu unapaswa kutokaribiana na watu walioambukizwa virusi vya corona.
USHAURI WA JUMLA: Jikinge na maambukizi ya virusi vya Corona kwa
Nawa mikono yako kwa maji tiririka kwa sabuni:
Ngao ya nje ya kirusi husaidia kirusi kiweze kuishi kwenye mazingira kwa muda pia husaidia kiweze kunata kwenye nyuso za vitu. Kutokana na kuwa na mafuta kwenye ngao. Unapoosha na mikono kwa maji pekee kirusi kitaendelea kunata bila kutoka kwa sababu ngao inafanya kirusi kuwa kama tone la mafuta
Molekyuli za sabuni zinapofika kwenye kirusi huivunja ngao ya nje ambayo imeundwa na mafuta na kirusi hubomoka na kutokuwa na uwezo wa kuishi tena. Pia ni muhimu kufahamu kwamba unaponawa na sabuni kwa muda wa sekunde 20 na kuendelea unatoa nafasi molekuli za sabuni kufanya kazi ya kuondoa virusi na chembechembe za uchafu kutoka kwenye sehemu zote za mikono pia hukupa muda wa kuosha sehemu zote
Vaa barakoa unapokuwa kwenye mikusanyiko
Barakoa (mask) ni kikinga pua na mdomo na ni nyenzo muhimu inayoweza kutumika kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya vimelea vya maradhi kupitia njia ya hewa. Kuna aina mbalimbali za barakoa ambazo huandaliwa kwa madhumuni tofauti. Zipo aina kuu tatu (3) za barakoa ambazo zinaweza kutumiwa ili kuzuia maambukizi ya vimelea vya maradhi kuenea zaidi au kumkinga mtu asipate maambukizi kutoka kwa watu wengine endapo yupo katika maeneo hatarishi. ya hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya.
Epuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima
Usiache kutumia dawa ulizopewa na madaktari
Hakikisha unatoa taarifa kituo cha afya unapohisi dalili zozote za kuzidiwa
Hakikisha unatembea na dawa zako muda wowote
MUONGOZO KWA WATU WENYE ULEMAVU WA MIGUU NA MIKONO
Kwa mtu mwenye ulemavu:
· Vaa barakoa mara kwa mara unapokuwa na watu wengine au unapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu
· Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni
· Epuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima
· Kaa umbali wa hatua tatu kutoka kwa mtu na mtu
· Epuka kugusa macho, pua na mdomo bila kunawa mikono
Kwa msaidizi wa mtu mwenye ulemavu wa miguu na mikono

· Vaa kikinga mkono (Glovsi) kila unapomsaidia mwenye ulemavu wa miko
· Hakikisha unavaa barakoa kila unapomuhudumia mwenye ulemavu wa viungo
· Jinsi Ya Kusaidia Wasioona Katika Kipindi Hiki Cha Mlipuko Wa Ugonjwa Wa Corona
· Mruhusu asiyeona akushike nyuma ya kiwiko cha mkono wakati anapohitaji msaada wa kusindikizwa au kuvuka barabara.
VIONGOZI WA DINI WANA NAFASI KUBWA YA KUIKINGA JAMII DHIDI YA MAAMBUKIZI YA #CORONAVIRUS
1: Hakikisha unatoa elimu kwa waumini kuhusu #COVID19
2: Hakikisha kwenye nyumba ya Ibada kuna sehemu ya kunawia mikono
3: Waumini wanawe mikono kwa Sabuni na Maji tiririka kabla ya kuingia kwenye Ibada
4: Idadi ya vipindi vya ibada iongezwe ili kuepusha msongamano
5: Waumini wakae umbali wa hatua 3 kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
6: Hakikisha Waumini hawapeani mikono kabla, baada au wakati wa Ibada
USHAURI WA LISHE KWA WATU WA MAKUNDI YALIYOKATIKA HATARI ZAIDI YA KUATHIRIWA NA UGONJWA WA #COVID19 NA JAMII KWA UJUMLA
Lishe bora na unywaji wa maji ya kutosha ni muhimu sana.
· Watu waokula mlo kamili huwa wana afya bora na huwa na mfumo kinga ulio madhubuti pia hupunguza uwezekano wa wa magonjwa wa kudumu na maambukizi. Unatakawa kula chakula bora kutoka shambani hasa vyakula visivyo vya viwanda. Unatakiwa kila siku upate vitamin, madini lishe, nyuzi lishe, protini na virutubisho vinasaidia mwili kuondoa sumu (antioxidants).
Kula chakula safi asilia ambacho hakijasindikwa kiwandani kila siku.
· Kula matunda, mboga za majani, maharagwe, karanga, nafaka hasa zisizokobolewa na vyakula kutoka kwa wanyama kama samaki, nyama, maziwa na mayai. Kila siku, kula matunda sawa na ujazo wa vikombe viwili, mboga za majani sawa na ujazo wa vikombe viwili na nusu, gramu 180 za nafaka, gramu 160 za nyama na maharage. Unaweza kula nyama nyekundu mara 1 au 2 kwa wiki, na nyama nyeupe kama kuku mara 2 hadi 3 kwa wiki
Kunywa maji ya kutosha kila siku
· Maji ni muhimu kwa uhai. Husafirisha virutubisho na kampundi muhimu kwenye damu, huratibu joto la mwili, husaidia kuondoa takamwili, husaidia kulainisha maungio ya viungo Kunywa maji wastani wa glasi 8 hadi 10 kwa siku Kwenye vinywaji maji ya kunywa ni chaguo sahihi lakini unaweza kutumia vinywa ji vingine kama juisi lakini dhibiti matumzi ya vinywaji vyenye sukari nyingi

Upvote
0