Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Tangu uvamizi wa Russia nchi Ukraine uanze Pro-Putin/Russia naweza kuwagawanya katika makundi matano
1. Wanaozungumzia huu uvamazi wa Urusi kwa upande wa Historia ila bahati mbaya historia imewapitia kushoto au ni ile historia waliyoisikia vijiweni tu kwa watu ambao hawajakanyaga hata darasa moja la Historia. Hapo utasikia NATO ilikuwa na makubaliano na Russia isijitanue kuelekea Urusi ikayakiuka, au kuna makubaliano/mkataba wa Russia na Ukraine isijiunge NATO . Hawa wanajitahidi ila Historia waliyo nayo ni uongo na hawana ushahidi wowote wa kihistoria.
2. Wanaozungumzia huu mgogoro kwa nadharia njama "conspiracy theories". Hawa wataongolea biolabs, ushoga, Covid, monkeypox, NWO na ujinga mwingine mwingi. Hawa ni wa kupuuzwa tu.
3. Wanaozungumzia huu uvamizi kama ushabiki wa Simba na Yanga tu. Hawa utasikia wanasema Ukraine sio Zimbabwe, NATO amezidiwa kila kitu na Russia, NATO kama mwanaume aingie vitani kupigana, dunia haiwezi kuwa na mbabe mmoja tu, Chechens wamekiwasha. Hawa wengi wao nafikiri ni watoto wa 2000 na hawajui hata maana ya vita nini.
4. Wanaompenda Putin na kushangilia uvamizi wake kwa sababu eti hata US au NATO huwa anavamia nchi nyingine na kwasababu hiyo taifa lingine lenye nguvu linaweza kufanya hivyo pia. Hawa ukianza kuwachumbulia case moja moja hoja yao inayeyuka kama povu
5. Wanaoamini NATO hasa US wame stage huu mgogoro kwa maslahi yao binafsi hasa ya kuuza silaha au wengine wanasema kuimuza Russia. Hapa utawakuta baadhi ya wasomi.