Makundi ya watu ambao huwezi kuwakwepa duniani

Makundi ya watu ambao huwezi kuwakwepa duniani

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
1. WANAFIKI*
Hili ni kundi la watu ambao wakiwa na wewe lakini wakiwa mbali na wewe wanaokusema vibaya au kukufanyia mambo mabaya. Watu kaka hawa hukupa changamoto na ni ngumu kumjua mnafiki kwa sababu watacheka na wewe pia wakiwa na wewe watafurahi huku nyuma ya pazia wakiwa wanakuwazia mabaya

2. MARAFIKI WA KWELI
Hawa ni watu ambao daima wako upande wako ili kusudi kukushauri mambo mazuri. Daima ni wenye kukuwazia mazuri wakiwa na wewe na hata wasipokua na wewe.siku zote huwa ni faraja na chachu ya maendeleo maishani mwako.

3. MAADUI
Hawa ni jumla ya watu ambao wenyewe ata uwepo au usiwepo wao ni kukuwazia mabaya.Hawa hukuchana ata mbele ya watu kwamba hawakupendi na wanakuchukia..Hawa hawaoni jau kukukandia ata kama upo mbele za watu. Hawa watu hujenga chuki kwako ambazo huwafanya wakuchukie ata ukifanya mazuri kwao

4. VIGEUGEU (TEAM UCHOYO )
Hawa husoma upepo kwanza ukiwa na hela wanakua rafiki zako ..lakini usipokua na hela tu wanakukataa. Hawa tabia zao ni kama za kupe ni kua na wewe kwenye raha tu. Vugeu geu wengi kazi zao ni kufaidika na wewe huku wao hawataki vya kwao ufaidike navyo.

5. TEAM SIKUJUI
Hawa hawanaga mda na mtu yoyote.Sio adui zako wala sio marafiki zako.Hawa hawanaga noma na mtu wala shobo na mtu.

6. TEAM ROHO MBAYA
Hawa wenyewe hawajawahi wazia mtu mazuri. Ata kama hakujui na wala humjui wao kukutana nao tu ni kama mkosi vile, hapa majambazi na wezi ndo kundi lao

7. TEAM HURUMA
Hawa ata kama huwajui wala hawakujui wao wanakuonea huruma.Ni wepesi kutoa msaada na kuhurumia watu.Wana amini katika upendo

8. TEAM HASIRA
Hawa ni watu ambao jambo dogo tu ! Hasira kama zote wao kila kitu ni kupanic tu.Hawachelewi kuanzisha uugomvi

9. TEAM KUJIKWEZA (MADHARAU CREW)*
Hawa wenyewe ni kukukatisha tamaa.Wanapenda kujiona wao ni wa faida kuliko wengine. Kazi yao ni kuwadharau wadau kwa kila wanachofanya.

Imeandaliwa na kimodomsafi toka Mwaro TV
🙏
 
Back
Top Bottom