Makusudi au bahati mbaya?

tinya

Member
Joined
Jan 4, 2010
Posts
77
Reaction score
30
Za leo! Za saa hizi,!
Jamani mwenzenu hata sielewi tunakoelelea, hivi kama kweli Tanzania kuna mgodi (sijui ndio mgodi au nimekosea) wa gesi asili (sijui nimepatia?) inakuwaje tunakosa umeme?
Au kama kweli Tanzania ina mazingira yanayofaa kutengenza umeme wa upepo jamani inakuwaje kweli tunakosa umeme!

Nimelazimika kuuza asikirimu na mabarafu baada ya kukosa ajira sasa umeme ndio huo nauona kwa kuhesabiwa masaa yaani unakatika saa 3 asubuhi unarudu saa 12 jioni kwa dakika kama 45 kisha unakatika mpka saa tano au sita usk huu si utani.

Uvumilivu unazidi kupungua karibu ntaandama mwenyewe kuelelea ikulu nikapate majibu.
 
Poleni sana wandugu kweli ni kero kubwa sana kukosa umeme
 
kuw ana gesi au upepo siyo suluhu ya kua na umeme. umeme au gesi ina nguvu ambayo inaweza kuzalisha umeme lakini hiyo nguvu siyo umeme. then kuna hitajika conversion ya hizo nguvu kuwa umeme. kwa hiyo hapo kinachogomba ni hicho cha ku-convert hizo nguvu kuwa umeme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…