Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Tangu kashfa mbaya kabisa ya maafisa wa Serikali kubainika wamesaini mikataba ya hovyo unaotarajia kuzipora bandari zote za Tanganyika, wahusika wamekuwa wanahangaika kuutetea uovu wao wakitoa hoja nyingi ambazo nazo haichukui muda kudhihirika ni uwongo.
1) Kwanza walisema eti kilichopelekwa bungeni haukuwa mkataba bali likuwa MoU. Ikadhihirika wazi kuwa ni uwongo. MoU, kwa upande wa Tanzania ilisainiwa na Mkurugenzi mkuu wa TPA mwezi February 2022. MoU haijawahi kupelekwa bungeni, na document hiyo ilisainiwa kwa usiri bila ya kutangazwa popote. Kwenye uwongo huu, wakaumbuka, wakabadilisha hadithi.
2) Wakasema mkataba haujasainiwa, utasainiwa baada ya kupitishwa na Bunge. Watu wema wakauvujisha mkataba ambao tayari ulionesha kuwa ulisainiwa na Rais Samia mwezi Octoba 2022. Hapa tena wakaumbuka. Wakabadilisha story.
3) Wakasema huo mkataba uliosainiwa na Rais Samia ni FRAMEWORK tu, mambo muhimu yatawekwa kwenye mikataba ya utekelezaji. Ikaja kudhihirishwa wazi kuwa FRAMEWORK contract au FRAMEWORK Agreement, kwenye mikataba, ndiyo mkataba mkuu unaotoa mwelekeo wote kwa mikataba ya utekelezaji. Ndiyo maana mkataba huu mkubwa ndio pekee uliopelekwa Bungeni. Mikataba midogo ya utekelezaji, haitapelekwa bungeni, itakuwa mikataba ya siri. Jambo la ajabu, mkataba huu mkuu hauna muda, na zaidi umeegemea kumlinda na kumneemesha DP bila kuwepo vipengere vya kulinda upande wa mwenye mali. Ni kama Serikali itakuwa inapokea maelekezo toka DP. Mkataba mkuu hauna muda, hauelezi DP itawekeza kiasi gani, hauelezi uwekezaji wa Tanzania ambao tayari umefanywa utaifanya nchi iwe na asilimia ngapi kwenye faida, ukiacha kodi ambazo zipo kisheria ambazo nazo DP hawataki wazilipe kama zilivyo, wanataka wao pekee yao walipe kodi pungufu. Kwa hiyo, kwenye hili tena, wameumbuka. Kwa wanaotaka kupanua uelewa:
"Framework Agreement is similar to a Master Agreement"
A 'framework agreement' is 'an agreement between one or more contracting authorities and one or more economic operators, the purpose of which is to establish the terms governing contracts to be awarded. It must entail price, period of the agreement and quantity envisaged. A framework agreement clarifies the responsibilities each party has. The agreement includes other areas like business ethics, privacy, access to property and networks and other social commitments. A framework Agreement is a real structure intended to serve as a guide for the building of something that expands the structure into something useful"
Hivyo, kama wanasema kilichosainiwa ni Framewoek, maana yake kilichosainiwa ni mkataba mkuu, mkataba kiongozi. Hakuna mkataba mdogo utakaokuja kusainiwa utakaokuwa na uwezo wa kukiuka yale yaliyopo kwenye mkataba mkuu. Mkataba huu mkuu umesainiwa na Rais. Mingine yote itakayofuata itasainiwa na watu wa chini kama vile mkurugenzi wa TPA au Waziri. Baada ya kushindwa kwenye hili, wamekuja na hadithi kuwa:
3) Kuna ubaguzi, kwa vile watu wengi wamesema kuwa waliosaini huu mkataba wa hovyo na wote waliohusika kwenye kadhia nzima, ni Wazanzibari. Sasa wanataka tuseme kuwa Rais Samia, Mbarawa na yule mkurugenzi wa bandari ya Dar, siyo Wazanzibari? Mbona Rais mwenyewe aliwahi kutamka kuwa yeye ni mzanzibari, ni Rais mwanamke. Badala ya kujibu hoja ilikuwaje Wizara isiyo ya mwungano akateuliwa Waziri mzanzibari, katibu mkuu Mzanzibari, wanakuja na vioja. Hatuhoji kabisa kwa nini Samia ni Rais wa Tanzania, kwa sababu ipo wazi kwenye katiba kuwa Rais anaweza kutoka upande wowote wa mwungano. Wameona wameshindwa kwenye hili, wamegeukia jingine:
4) DP wanapingwa kwa sababu ni waislam. Na hii wanaisema kwa kuamini, hoja hiyo ikikubaliwa, basi wale waislam wa Tanganyika ambako bandari zake zinaenda kuporwa, wataachana na maslahi ya Tanganyika yao, na kuungana na waporaji na makuwadi wao kwa kuisaliti Tanganyika yao. Wanataka kutaka kuwaaminisha watu ule mkataba wa hovyo ni mkataba wa dini ya kiislam na Tanzania. Hii ni sawa na kumtaka muislam mzuri aungane na jambazi kwa vile tu jambazi yule ni muislam. Kuna majambazi yenye majina ya kiislam au ya kikristo, lakini katu matendo yao ya hovyo wasiyageuze kuwa ndiyo uislam au ndiyo ukristo. Ukienda magerezani utawakuta wafumgwa wengi wenye majina ya Mohamed, Shaban, John au Pascal, lakini hiyo haiashirii uislam au ukristo unatumikia kifungo jela. Hili nalo wameshindwa.
Baada ya yote kugonga mwamba, wamebaki wanapiga kelele, mara oh, natoa onyo kwa Dr. Slaa, mara oh kama Tanganyika hawataki muungano tugawane mbao, n.k. Hizi ni hadithi za kawaida. Hakuna uovu ambao ulikosa uungwaji mkono kutoka kwa waovu wenzao.
Kama DP wapo tayari kuikiri uovu wao na dhamira yao chafu kama ilivyoonekana kwenye mkataba ule hovyo, na kwamba wapo tayari kujadiliana kwa mkataba wazi ili wawekeze kwenye biashara ya bandari, waje kwa uwazi, majadiliano yaanze upya bila kuwashirikisha Mbarawa na kundi lake, wala wale wabunge waliopokea rushwa. Na wale wanahabari waliokula hongo wapigwe marufuku kuongea au kuandika chochote kuhusiana na bandari. Lakini pia sheria yetu hutoa msamaha kwa mtu au taasisi iliyolazimishwa na mazingira yaliyopo kutoa rushwa. DP itoe ushirikiano kwaajili ya kuwaadhibu wabunge, wanahabari na maofisa wa serikali waliopokea hongo.