Makuwadi wanahangaika kuhalalisha mkataba mbaya wa DP World lakini kila mahali wanaangukia pua

Bams bams bams... Wee haya ngoja waje akina Lord denning covax na choiceVariable moto watauwasha hapa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Moto wa makuwadi ni kama moto wa majani ya mchongoma, hauyeyushi chuma.
 


Najua unaitaja CCM ili wanaCCM wasiuone uozo, waishie kusema kuwa tunaipigania CCM.

Umechelewa. Ujue kuwa kuna wanaCCM wengi wamechukizwa sana na chama chao kutumika kama daraja la kwenda kuiuza Tanganyika.

Unajidanganya sana. Ufahamu kuwa ni wanaCCM ndio waliokuwa wa kwanza kufadhaishwa na mkataba huu wa hovyo. Tena ni wanaCCM viongozi ndio waliovujisha mkataba huu wa hovyo kwa wananchi na vyama vya upinzani.
 
Itanichukua muda mrefu sana sana kuamini kama nchi ina Raisi,spika na jaji mkuu.
 
Wanahangaika sana sana. Huyu mama anatakiwa aondolewe.
 

Hapo unasema. Mkataba wa "hovyo " halafu huuoneshi ambao siyo wa "hovyo" ukoje.

Sisi tunaoujuwa huu hapa 👇🏾 tuoneshe huo uhovyo wako uko wapi? Bofya chini hapo 👇🏾



Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Hizi kelele za bandari zitapita tu, lkn km ni kuuzwa hiyo bandari ishauzwa
 
madalali na makuwadi ya dpworld tunawaagiza mkawape taarifa hao mnaowakuwadia kuwa wakija tutawashughulikia kama wezi mnadani.
Maandamano tu mmeingia mitini. Acha tusubiri tuoni nani huyo wa kuwashughulikia
 
Safi sana kwa uchambuzi makini! DP world wakae wajue Katiba ya Jamhuri ya Muungano inawapa wananchi mamlaka juu ya serikal! Wananchi wakikataa serikali lazima ifyate mkia! Kama awaamini waache walazimishe wao na vibaraka wao wakiongozwa bi domo kubwa waone nguvu ya umma
 
Kelele za chura tu hizo.
Bandari ndo ishauzwa, haya sasa twasubiri tuone mtakalofanya zaidi ya kuhangaika tu nyuma ya keyboard
 
Sawa mkataba wa muda gani?
 
nikitafakari issue za loliondo, moyo hua unaniuma sana. kwahiyo lile ni eneo la uarabuni au la Tanganyika, na kama walikuwa ni wawekezaji, mkataba wao ulitakiwa kuisha lini. ukiunganisha na hili la bandari unaconclude kwamba mwarabu hafai.
 
Inatia uchungu sana!
tumepigwa alafu nashangaa kuna watanzania wengi hawaelewi kwamba wamipigwa
 
Kelele za chura tu hizo.
Bandari ndo ishauzwa, haya sasa twasubiri tuone mtakalofanya zaidi ya kuhangaika tu nyuma ya keyboard
Mkuu umehaidiwa na wahusuka kukupatia ajira kwa ujira mnono nini? Hongera zako kwa utetezi wako kwa DP-W Z kwa nguvu zako zote; utazani wewe ni Mrundi wa Burundi
 
Toa kasoro kwenye huu mkataba kama wewe ni Mzalendo sio porojo tu
Tulikwishausoma wote kabla haujafika hata bungeni.

Ulichokileta hapa siyo nakala ya mkataba bali ni tafsiri yako kwa Kiswahili.

Weka mkataba halisi ambao hawajawahi kuuona ili wausome. Mimi sihitaji kwa sababu niliuona hata kabla haujafika bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…