Makuzi: Serikali vs Familia

Makuzi: Serikali vs Familia

Petu Hapa

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2008
Posts
714
Reaction score
57
Niliahidi katika thread mbili tofauti nitaandika kuhusu malezi ya watoto kujaribu kuelewa majukumu ya serikali na ya familia ni yapi katika makuzi ya mtoto. Katika tafiti nyingi inaonyesha kwamba uwekezaji katika watoto kupitia familia na serikali vinafaida katika kujenga nguvu kazi ya taifa, na familia kujikwamua katika umaskini. Lakini kwa kiasi kibwa serikali ya tanzania imekuwa ikishutumiwa kwa kushidwa kulinda watoto kwa kiwango kizuri.

Ni dhahiri, katika makuzi ya mtoto familia ndiyo inayopaswa kulinda na kumkuza mtoto katika mazingira ya upendo na uchochozi wa udadisi, kwa kutumia imani mbalimbali za dini, tamaduni na elimu. Lakini kwa wakati huo huo, serikali ndicho chombo kinachotegemewa kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa katika aina ya makuzi tofauti. Ni jinsi gani ambavyo serikali na familia vinafanya kazi pamoja ni swala ambalo tunapaswa kulijadili kwa kujiuliza maswali yafuatayo.

Je ndani ya makuzi ya watoto wa kitanzania, jukumu la familia ni lipi? Je jukumu hili linatambuliwa kikatiba? Wazazi wanatimiza majukumu hayo?

Je jukumu la serikali ni lipi katika kuhakikishwa haki za watoto zinalindwa? Vyombo gani vilivyopo vinavyolinda maslahi ya watoto? Je kunasheria gani ambazo zinalinda watoto? Je serikali inatumia bajeti kiasi gani kuhakikisha maslahi ya watoto katika elimu, michezo, na afya?
 
Last edited:
Back
Top Bottom